Social Icons

Monday 15 July 2013

HADITHI : HAIKUWA BAHATI YANGU SEHEMU YA KWANZA

 Hiki ni kisa ambacho kinamuhusu kijana mmoja ambaye alikuwa na ndoto za mbele na kutimiza malengo yake , lakini ni nini kilimtokea na ilikuwaje kuwaje ungana nami hapa.


Naomba Radhi kwa baadhi ya sehemu mchapishaji kukosea kuandika


Na Fredy Njeje

Joseph ni kijana ambaye amezaliwa katika familia ya Kikulima huko Mbozi, wazazi wake waliishi katika maisha ya kifukara sana kutokana na ukosefu wa Elimu, hata hivyo waliona ni muhimu kwa kijana wao apate elimu ya kutosha. Waliamua kumsomesha kwa chochote 
walicho kuwa nacho ilimradi mwanao apate elimu ya msingi na baadae aje awakwamue kutoka katika hali ya umasikini. Joseph alikua mtoto wa pekee katika familia ya mzee Simbeye.

Ilipofika mwaka 1984 wakati Joseph alipotimiza miaka 10 wazazi wake waliamua kumuandikisha katika shule iliyokuwa jirani na kijiji ambacho waliishi kilichoitwa Mbozi Mission shule iyo iliitwa Mwenge wilayani mbezi ambayo makao makuu yake ni Vwawa. Joseph alikuwa ni moja ya wanafunzi waliopenda sana Shule maendeleo yake yaliwafanya walimu wampende pia kutokana na juhudi zake alipendwa na rafiki zake pamoja na wanakijiji wote

Ilipofika mwaka 1990 Joseph alimaliza elimu yake ya Msingi Kitendo ambacho kiliwafurahisha wazazi wake. Baada ya miezi mitatu matokeo yalitoka na Joseph alikuwa ni mmoja kati ya vijana wachache waliochaguliwa  kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Mbeya . Kutokana na Furaha waliokuwa nayo walitamani kufanya sherehe kwa ajili ya kijana wao wakashindwa kutokana na hali ya ufukara waliokuwa nayo

Wazazi wake walipokea Taarifa ya kuchaguliwa mwanao kwa furaha kubwa na walifanya kila jambo ili mtoto wao aweze kuendelea na elimu ya Sekondari. Baada ya siku kadhaa kupita na alipo karibia kwenda shule wazazi wa Joseph walikuwa bado kabisa hawajapata pesa na hawakuelewa watamsaidiaje. Jioni ilipofika wazazi wake ilibidi wamkalishe chini na kumueleza hali halisi. "Mwanangu Joseph sisi wazazi wako tumefurahi sana ya kuwa umechaguliwa kuendelea na masomo yako ya Sekondari, lakini tunasikitika sana tumefanya kila tuwezalo tumeshindwa kabisa kupata namna ya kufanya itakayo kuwezesha kuendelea na masomo ya sekondari" alisema baba yake Joseph, aliongea akiwa na huzumi kubwa. Baada ya Joseph











 Itaendelea... Endelea kufuatilia kisa hiki cha kusisimua..

1 comment:

Anonymous said...

simuzi nzr lkn mnaikatisha vp ln tuipate tena