Social Icons

Thursday, 29 December 2011

Airtel wakabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya MZUKA







Afisa
Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Jane Matinde
(kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Samsung Tablet kwa, Edith
Mbenna (kulia) ikiwa ni zawadi baada ya kuibuka

mshindi katika promosheni ya mzuka wa Airtel . katikati yao ni Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akishuhudia makabithiano hayo
katika ofisi kuu za Airtel, Dar es Salaam.








Afisa
Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Jane Matinde
(kulia) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Samsung double line kwa Ariff
Warri (kushoto) ikiwa ni zawadi baada ya kuibuka

mshindi katika promosheni ya mzuka wa Airtel . katikati yao ni Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akishuhudia makabithiano hayo, hafla
ya makabidhiano iliyofanyika Airtel











Meneja
Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Jackson
Mmbando (kulia) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Samsung Galaxy ii kwa
sandra Mwasenga (kushoto) ikiwa ni zawadi baada ya

kuibuka mshindi katika promosheni ya mzuka wa Airtel . katikati yao
anayeshuhudia makabithiano hayo ni Jane Matinde Afisa uhusiano wa
Airtel,hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo Airtel






Meneja
Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Jackson
Mmbando (kulia) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Samsung Tablet kwa
Pelagia Weiss (kushoto) ikiwa ni zawadi baada ya kuibuka mshindi katika
promosheni ya mzuka wa Airtel . katikati ni Jane Matinde Afisa
uhusiano wa Airtel

Wednesday, 28 December 2011

Mkesha Mkubwa Kitaifa Waja Usiku Wa Mwaka Mpya

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkesha Mkubwa – Dua maalum kwa Taifa askofu Godfrey Emmmanuel Malasi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mkesha mkubwa wa kuliombea taifa utakaofanyika katika uwanja wa taifa Desemba 31,2011 ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete. Wengine ni Viongozi wa kamati hiyo kutoka Umoja wa makanisa ya Kikiristo Tanzania (Tanzania Christian Fellowship of Churches).
Viongozi wa mkesha mkubwa wa kuliombea taifa (waliosimama mbele) wakifanya maombi maalum kwa waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kuitumikia jamii kwa uadilifu kutokana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.Maombi hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam. Picha na Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
--
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
28/12/2011.
Umoja wa makanisa ya Kikiristo Tanzania (Tanzania ChristianFellowship of Churches) umeandaa mkesha mkubwa kwa ajili ya dua maalum kwa taifa kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa kulivusha taifa katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine ambapo mgeni rasmi katika mkesha huo atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkesha mkuu kutoka Tanzania Christian Fellowship of Chrches Askofu Godfrey Emmmanuel Malasi amesema watanzania wanapaswa kujua Mungu anakusudi gani na taifa la Tanzania katika kipindi hiki ambacho Taifa limetimiza miaka 50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine na kutoa wito kwa kila mtanzania kufanya kazi kwa bidii na kushiriki katika uchumi wa taifa.
Amesema serikali inazo sera nzuri za kuweza kuwamilikisha wananchi rasilimali ziliizopo nchini ili waweze kuishi maisha bora na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kutambua majira na wakati uliopo sasa wakati taifa linapoanza miaka 50 mingine ya uhuru kwa kuzitumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
“Kila mmoja anapaswa kushiriki na kushirikishwa kikamilifu katika uchumi wa taifa letu ambalo sasa limemaliza miaka 50 ya uhuru, kila mtu anapaswa kutambua nafasi yake, tusikae kwa kubweteka, tusikae kwa kulalamika kila mtu ajue ni wakati wa kumiki na kurithishwa rasilimali zilizopo katika taifa hili”
Amesema mwaka huu dua maalum kwa taifa litafanyika katika mikoa 14 ya Tanzania ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza,Kilimanjaro, Singida Iringa, Mbeya ,Iringa, Kagera, Dodoma, Ruvuma, Tabora,Tanga na visiwa vya Zanzbar na Pemba.
Amefafanua kuwa katika mkesha huo viongozi mbalimbali wa taifa ,vyama vya siasa na balozi mbalimbali zipatazo 37 zilizopo nchini zimearikwa kushiriki mkesha huo na kuongeza kuwa tayari baadhi ya balozi zimethibitisha kushiriki mkesha huo.
Kuhusu maadalizi ya mkesha huo askofu Godfrey Malasi amesema yanaendelea vizuri na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika dua hiyo maalum na kuongeza kuwa mkesha huo utaambatana na tukio maalum la watoto 50 kusimama uwanjani na kutamka maneno ya kupokea miaka 50 ijayo ikiwa ni ishara ya kupokea kizazi huru cha watanzania.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya mkesha mkuu wa Taifa Askofu Keneth Damas ameipongeza serikali kwa kuwa na msimamo wa kupinga suala la ndoa za jinsia moja (ushoga) katika mikutano ya kimataifa iliyofanyika hivi karibuni na kuuita uamuzi huo kuwa ni ushindi mkubwa kwa taifa la Tanzania na watu wake katika kuheshimu utu na utamaduni wa taifa na uukataaji wa vitendo vya udhalilishaji na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini wataendelea kuonya na kufundisha watu wajue athari za dhambi hiyo.
“Sisi kama viongozi wa makanisa katika nchi hii tunapinga kwa nguzu zote vitendo vya ushoga ndani ya taifa letu, vitendo vya ushoga ndivyo vilivyosababisha Sodoma na Gomora kuchomwa moto kwa kuwa vilimchukiza sana Mungu, Sisi kama viongozi wa dini katika kizazi chetu na vizazi vijavyo hatutaki kufikia hapo na kuona taifa letu likichomwa moto”



Monday, 26 December 2011

Wachezaji Yanga walia njaa

Timu ya Yanga

Ikiwa inakabiliwa na ushindani mkali katika kampeni yake ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na pia mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, programu za mazoezi ya Yanga inashindwa kutekelezeka kikamilifu kutokana na wachezaji wake kutopata mishahara yao ya miezi miwili.
Mishahara hiyo ambayo wachezaji wanadai ni ya mwezi Novemba na Desemba, ambao umeambatana na sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata ni kwamba mbali na wachezaji hao, pia wafanyakazi wengine walioajiriwa na klabu hiyo hawajalipwa kwa muda wa miezi mitatu sasa.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa hali hiyo ya ukata imechangia mambo mengi kutofanyika kama ilivyotarajiwa ikiwemo kuvurugika kwa programu ya mazoezi.
"Hali ni mbaya, klabu haina pesa, mambo mengi hayafanyiki kama ilivyokusudiwa, tunajaribu kufanya kila linalowezekana ili kutatua tatizo hili linalotukabili," alisema mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Aliongeza kuwa kukosekana kwa fedha kutoka kwa aliyekuwa mfadhili wao na mapato madogo ya mlangoni yaliyokuwa yakipatikana katika mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi ndio sababu nyingine iliyofanya klabu yao ikose fedha za kujiendesha.
CHANZO: NIPASHE

Bonite Botllers Co-ltd ya Moshi yatoa msaada wa soda....


Kampuni ya kutengeneza vinywaji baridi ya Bonite ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro imetoa msaada wa soda kreti kumi, kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya serikali ya mkoa wa Singida, kwenye picha mganga mkuu wa mkoa Singida Dk.Robert Salim (kulia), akipokea msaada huo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Bonite, tawi la Singida.
Mwakilishi huyo alisema msaada huo ni kwa ajili ya wagonjwa wote waliolazwa katika hospitali hiyo, ili nao wajione sawa na binadamu wengine wazima, waliopo kazini, majumbani na safarini.
Na Elisante John

Saturday, 24 December 2011

NGOMA AFRICA BAND YATOA SALAM ZA RAMBI RAMBI KWA WAHANGWA MKOA WA DAR-ES-SALAAM,

Bendi ya muziki wa dansi Ngoma Africa band aka FFU yenye makao yake Ujerumani,

Inaungana na watanzania wote kwa kutoa pole na salam za rambi rambi kwa wahangwawaliopatwa na maafa ya mafuriko ya maji mkoa wa Dar-es-salaam.Maafa hayo yalisababishwa na mvua kubwa,yamepoteza maisha ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa wa makazi ya jamii na mali zao,pamoja na barabara mkoani Dar-es-salaam.
Tunaotoa pole kwa wahangwa wote,Mwenyezi Mungu atupe uvumilivu na mshikamano katika kipindi hiki kigumu.


Umoja ni Nguvu

www.ngoma-africa.com


NGOMA AFRICA BAND YATOA SALAM ZA RAMBI RAMBI KWA WAHANGWA MKOA WA DAR-ES-SALAAM,

Bendi ya muziki wa dansi Ngoma Africa band aka FFU yenye makao yake Ujerumani,

Inaungana na watanzania wote kwa kutoa pole na salam za rambi rambi kwa wahangwawaliopatwa na maafa ya mafuriko ya maji mkoa wa Dar-es-salaam.Maafa hayo yalisababishwa na mvua kubwa,yamepoteza maisha ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa wa makazi ya jamii na mali zao,pamoja na barabara mkoani Dar-es-salaam.
Tunaotoa pole kwa wahangwa wote,Mwenyezi Mungu atupe uvumilivu na mshikamano katika kipindi hiki kigumu.


Umoja ni Nguvu

www.ngoma-africa.com


Friday, 23 December 2011

VODACOM TANZANIA YATOA MSAADA KWA WAADHIRIKA JIJINI DARES SALAAM...!!!




Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadiq Meck Sadick ksuhoto akiwa na Mbunge wa Kinondoni Bw. Iddi Azan akipokea magodoro kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule .Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Vodacom Bi. Najengwa Mbagga. Vodacom imekabidhi magodoro 430, mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 30 milioni kusaidia kambi za waathirika wa maafa ya Dar es salaam.






Wafanyakazi wa Vodacom wakiwa katika picha ya pamoja




Sehemu ya shehena ya magodoro 430 yaliyotolewa msaada na Vodacom kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam yakiwa tayari kukabdhiwa kwa kamati ya maafa ya mkoa wa Dar es salaam. Mbali na magodoro Vodacom ilikabidhi pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.




Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakishusha sehemu ya magodoro 430 yaliyotolewa na kampuni hiyo katika kambi ya waathirika wa maafa ya Dar es salaam ya Mchikichini. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.




Sehemu ya watoto wanaoishi katika kambi ya waathirika ya maafa ya Dar es salaam katika kambi ya shule ya msingi Mchikichini wakiwa na magodoro yaliyogawiwa na Vodacom kwa waathirika wanaoishi katika kambi hiyo. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation.




Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Bi. Beatrice Makangara kushoto na Bi. Jacqueline Tarimo wakiwaongoza wenzao kuelekea kugawa magodoro 430 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.




Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadiq Meck Sadick kushotoakiteta jambo na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule .Vodacom imekabidhi magodoro 430, mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 30 milioni kusaidia kambi za waathirika wa maafa ya Dar es salaam.





***






*Yatoa magodoro, mablanketi na vyakula kwenye kambi

Dar es salaam Disemba 23, 2011.



Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom leo imekabidhi msaada wenye thamani ya shilingi 30 Milioni kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam wanaoishi katika makambi maalum yaliyofunguliwa kuwawezesha kujihifadhi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya.


Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule amekabidhi msaada huo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadik Meck Sadiq ukijumuisha magodoro 430 mablanket 800,na vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni kumi. "Tumeshtushwa sana na hali halisi ya maafa yaliyotukumba jijini Dra es salaam, tumefika hapa kuendeleza utamaduni wa Vodacom kwa kuonesha upendo na kuwa karibu na wananchi katika nyakati za raha na shida."Alisema Mwakifulefule.


Vodacom imekabidhi msaada huo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ambao umekuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za maendeleo katika jamii na pia kufariji waathirika nyakati za maafa. "Mafuriko haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi kuwahi kutokea Dar es salaam katika muda wa miaka mingi iliyopita na hivyo ni wazi athari zake ni kubwa, tunatoa pole kwa wote waliopoteza watoto, ndugu na jamaa na wale walionusurika tunawatakia afya njema na faraja katika wakati huu mgumu wa maisha wanaoupitia"Aliongeza Mwakifulefule Adha kampuni hiyo imetangaza pia fursa kwa wateja wake na wa wananchi kwa ujumla kuungana na Menejimenti na wafanyakazi wake kuchangia walichonacho kupitia nambari maalum ya maafa ya Vodacom Red Alert na kwa njia ya m-pesa.


Kupitia nambari ya Red Alert wananchi wanaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi - SMS wenye neno "MAAFA" kwenda nambari15599 na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.


"Mahitaji kwa wenzetu waliothirika ni makubwa. Tuna imani kuwa wote kwa pamoja tutaonesha umoja, upendo na mshikamano wetu wa kitaifa unaojenga tunu ya Utanzania wetu kusaidia wenzetu ambao kwa wakati huu wapo katika mashaka makubwa wakihitaji faraja ya kila aina". Amesema Mwakifulefule.


Michango yote itakayokusanywa kupitia nambari hizi itawasilishwa kwa kamati ya Maafa ya mkoa kuongeza nguvu katika juhudi za kuwasaidia waathirika na kwamba utaratibu wa kuwapatia taarifa wachangiaji utakuwepo.


Aidha kampuni ya Vodacom Tanzania imevipongeza kipekee vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa juhudi kubwa za uokozi kwa kushirikiana na wananchi hatua ambayo imesaidia kunusuru maisha ya maelfu ya watu. Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa


*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa. Hatua ya 2: Chagua 4 - Lipa Bili


Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni - weka namba 155990 Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu - weka namba yako ya simu Hatua ya 5: Weka kiasi - ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri Hatua ya 7:Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia. Mwisho.
















Monday, 19 December 2011

Hot nuuz: Sakata la mafuta lachukua ukurasa Mpya yapatikana sehemu moja tuu. vituo vyagoma kuuza mafuta


 Baadhi ya Magari yakiwa yamepanga foleni ndefu yote yakiwahi  mafuta
 Mwandishi wa habari akijitahidi kumsaidia mdau baada ya kuishiwa na mafuta eneo la Mlimani City
 Watu wengi wakiwa wamejazana wakingojea huduma ya kupata mafuta eneo ilo la kituo cha mafuta cha Total karibia na Mlimani city
 Bajaji ikiwa imeishiwa mafuta

 Kijana akiwa amechanganikiwa baada ya kutaka kugongwa wakati wa harakati za kusaka mafuta


 Boda boda ikiwa mzigoni kupeleka mafuta eneo husika

 
 Gari la Mafuta likiwa limewasili kwa ajili ya kuongeza mafuta baada ya kwisha eneo hilo
 Mdau wa Business week akiwa anaweka mafuta baada ya kumwishia
 Boda boda wakiwawanakimbilia mafuta
 Mdau akiwa anavuka bara bara kwa kasi baada ya kupata mafuta
Ikiwa ni siku ya nne sasa hali ya mafuta yazidi kuwa ni tete zaidi