Bofya hapa Chini
Monday, 30 April 2012
Vijimambo vya Ughaibuni Mtaani Hummer Lakatiza mtaani na kusababisha usumbufu
Hapa lilikuwa kabla lilikuwa nyuma kidogo
Hapa Hili dude limepanga Foleni huku likizuia magari madogo ambayo yalikuwa yanakwepa
Hapa Linaendelea kutafuta kaupenyo
Hapa limepata ka upenyo lakini Basi limeziba hapo.. Jamaa akaanza kutoa maneno makali.
********
Kikubwa hapa haya magali yanapo katiza mtaani yanasababisha usumbufu mkubwa sana
Maandalizi ya Redd's Miss Ustawi wa Jamii yapamba moto
Washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss Ustawi wa Jamii 2012 wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu wao,Mary Boniface (katikati) wakati wa mazoezi ya kujiandaa na shindano lao linalotaraji kufanyika siku ya ijumaa (Mei,4 2012),ukumbi wa Maisha Klab jijini Dar es salaam.
Warembo wa Redd's Miss Ustawi wa Jamii 2012 wakiwa kwenye pozi.
Mwalimu wa Dansi kwa Warembo wa Redd's Miss Ustawi wa Jamii 2012 akitoa somo kwa warembo hao.
Picha kwa hisani ya Mtaa kwa mtaa Blog
Picha kwa hisani ya Mtaa kwa mtaa Blog
HII KALI KULIPO :MSANII RICH ONE AFIKISHWA POLISI KWA KUJIFANYA ALLY KIBA MUDA MCHACHE ULIO PITA
Rich One mwenye t shirt nyekundu msanii wa TMK WANAUME HALISI akiwa kafikishwa polisi tayari.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya,Rich One amefikishwa kwenye kituo cha polisi Msimbazi Dar es salaam muda mfupi uliopita kwa tuhuma za kutapeli, kula hela za watu akijifanya yeye ni mwimbaji Ally Kiba ambapo inaaminika yeye (Richone) alifanya utundu ambao Kiba akipigiwa simu haziendi kwake, zinakwenda kwenye simu ya Rich ndio anazipokea na kula hizo pesa za show.Zaidi sikiliza baadaye kipindi cha Amlifaya ya Clouds FM
Habari kwa hisani ya Millardayo.com
SHOO YA KIHISTORIA YA DIAMOND NDANI YA DAR LIVE! AKONGA NYOYO ZA MASHABIKI KIBAO
Ilikuwa ni shoo iliyopandisha mzuka wa mashabiki kupita kawaida.
Diamond akifanya vitu vyake, akiwa amevalia staili ya US Marine.
katika shoo zote za Dar Live, Diamond amevunja rekodi ya idadi ya mashabiki
licha ya mvua kunyesha wakati fulani, mashabiki hawakukubali kuondoka bila kumuona Diamond!
PICHA: Richard Bukos, Issa Mnally/GPL.
PICHA: Richard Bukos, Issa Mnally/GPL.
Ukitaka salama kwenye mapenzi, usifanye makosa haya

Ni Jumatatu nyingine ambayo tunakutuna tena kwenye uga huu tunaoutumia kupeana elimu ya masuala yahusuyo mapenzi. Leo tunaendelea pale tulipoishia wiki iliyopita kuhusu makosa ambayo hupaswi kuyafanya kwenye uhusiano wa kimapenzi.
KUSHINDWA KUSOMA ALAMA
Zipo alama muhimu ambazo ni vema kuzijua na uzibaini kwa mwenzi wako kabla hujazama kwenye dimbwi la mapenzi. Bahati mbaya wengi hutawaliwa na papara, matokeo yake hushindwa kubaini vitu ambavyo vinaweza kumfanya apate uelekeo wa uhusiano wake.
Katika pointi hii, nashauri watu kwenda kwa mwendo wa kinyonga badala ya kupiga mbizi bila kujua kina cha maji. Kusoma alama muhimu kwa mwenzi wako mapema ni sawa na kutegua kitendawili. Itakusaidia kujua kama kweli uliyenaye ana mapenzi ya kweli au anaweza kuwa laghai.
Wengi wanapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi hueleza kuwa wanapenda, tena huweka wazi kuwa hisia zimeanguka kwa wale wanaowapenda. Hata hivyo, huacha mambo mengi ndani ya uvungu wa nyoyo zao. Wewe utakuwa mshindi, endapo utaweza kumsoma mwenzi wako na kumuelewa kinagaubaga.
Pointi hapa ni kuwa mwanzo kabisa wa uhusiano, yapo mambo mengi ambayo kila mmoja hujitahidi kuyazungumza. Hiyo huita kujiweka wazi lakini imethibitika kitaalam kwamba maelezo ambayo hutolewa ni asilimia 40 tu, zilizobaki hufichwa. Asilimia 60 zilizobaki utazifichua kwa kusoma alama muhimu.
Nyongeza ni kwamba mara nyingi wengi hujitahidi kusema uongo mwanzoni mwa uhusiano. Hata kama mtu anapenda lakini hudanganya hili na lile pengine kwa hofu, tahadhari au kama pointi ya kushinda penzi. Mantiki hapa ni kukutaka uwe makini na umsome mwenzako kwa undani kabisa.
Katika kipengele cha kusoma alama muhimu, kuna vitu vya msingi vya kuzingatia ambavyo ni hivi vifuatavyo;
1) Jamii: Mwenzi wako anasimama vipi na jamii yake? Usiingie kichwakichwa kwenye mapenzi na mtu ambaye hata jamii yake inamuona ni tatizo. Vilevile, yule ambaye ni muoga inabidi uanze kumtia wasiwasi mapema. Ni kwa ajili ya maisha yako, hivyo ni vema kuchangamka.
Hutakiwi kugundua muda umeshapita kuwa mwenzi ana tabia usizopenda. Mapema msome na umuelewe. Chunguza msimamo wake kwenye jamii, anavyojiamini, je, anaonesha kuwa na dira ya maisha. Kama hana uelekeo, unatakiwa kuachana naye haraka.
2) Hisia: Zisome hisia zake, je ni mtu anayejali? Unatakiwa kujua kama hisia zake zipo karibu kwa kiasi gani. Atakapotakiwa kukutimizia haki yako ya faragha, atakuwa tayari kwa wakati? Ni aibu mmeshakuwa na uhusiano kwa muda mrefu ndiyo unaanza kulalamika kwamba mwenzi wako hakutimizii huduma ya uwanja wa wawili.
Lingine kwenye hisia, unatakiwa ujifunze kujua kama mwenzi wako ni mtu wa kulipuka au kinyume chake. Inawezekana ni kweli mwenzi wako anakupenda lakini akawa ni mtu wa jazba, tatizo dogo ‘anapaniki’ utadhani nyoka aina swila, kakanyagwa mkia. Mjue halafu umpime, je, unaweza kumvumilia? Jiridhishe mara mbili, vinginevyo bwaga manyanga.
3) Muonekano: Ni kipengele kidogo muhimu ndani ya kifungu cha kushindwa kusoma alama kama sehemu mojawapo inayowafanya wengi kufanya makosa kwenye uhusiano. Muonekano si suala la baadaye, inatakiwa mapema sana umtathmini halafu ujiridhishe kama anakufaa au kinyume chake.
Ni aibu umeshaingia kwenye uhusiano, halafu baadaye unamsaliti mwenzi wako na kuanza kuwatolea macho wale ambao unaona ni wazuri zaidi. Hakikisha kwamba mwanzo kabisa kwenye uhusiano wako, unajiridhisha kuwa anao mvuto unaokutosha.
Itaendelea wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
KUJITOA KWA MWANA-FA TFU KWA MUEPUSHIA BALAA LA ANTI-VIRUS VOL 3
Mwanamuziki wa Hip hop mwenye mafanikio ya aina yake katika industry ya muziki wa kibongo, Hamis Mwinjuma a.k.a MwanaFA ameondolewa kwenye list ya watu ambao walipaswa kuchanwa kwenye volume three ya Anti-Virus ya Vinega.
MwanaFA ambaye alikuwa centre ya michano katika volume iliyopita iliyopata mafanikio makubwa, safari hii ameondolewa kwenye hiyo list baada ya kujitoa rasmi TFU ambayo ni kampuni ya wasanii yenye dhamana ya kusimamia inayosemekana studio iliyotolewa na mwenye nchi yake. TFUama Tanzania Fleva Unit na ilipata wakati mgumu sana pale Mh Sugu alipoilipuwa bungeni huku umati wa Tanzania ukikodoa macho kwenye kideo.
Akizungumza na KaribuNdani Kinega kiongozi Peenlawyer amesema Mwana FA sio target tena kwani kashajitoa TFU ila moto utawaka kwa Kusaga, Nchimbi na utawaka zaidi kwa Ruge, mameneja masoko, Kili Awards na baadhi ya watangazaji ambao wamekuwa chachu ya rushwa na unyanyasaji wa wasanii..
Volume 3 iko njiani na kinachofanywa kwa sasa ni kujipanga ili kuangalia muda muafaka wa kudondosha hiyo mix-tape.
Habari kwa Hisani ya Chuma Blog
TUKIO LA SAFARI YA DIMOND KUELEKEA DAR LIVE, MBAGALA NA HELIKOPTA.
Huyu ndiye Diamond mwingine hakunaga, akielekea kupanda helikopta kwenda viwanja vya Dar Live kufanya makamuzi jana Jumapili, 29 April 2012
Diamond akiwa na rubani wake wakielekea kwenye helikopta
Hapa nimemkubali maana hakuna kitu muhimu kama kujikabidhi mikononi mwa Mungu kabala ya kufanya jambo lolote
Yes Sir, Salute
Mashabiki full kupagwa baada ya kusikia helikopta ikiwasili na star wao
Helikopta ikingia uwanjani hapo chezeaaa
Dar Live palikuwa hapatoshi
Ilikuuwa patashika kwa mashabiki wa Diamond, Bless them
Helikopta ikamshushua ka kuondoka zake
Diamond akimsalute rubani wake na Mwenyezi Mungu kwa kumfikisha salama
Ni showbiz kwa kwenda mbele, hapa akisalimiana na mashabiki wake
Diamond akishuka kwenye gari tayari kwenda kufanya makamuzi
Picha kwa hisani ya Issa Mnali & Erick Everist (GPL)
Sunday, 29 April 2012
Simba Haooo Robo Fainali yashinda kwa magoli matatu kwa bila
Leo wamewatandika Al Ahly Shandy 3-0! Kwao Sudan tunahitaji sare tu, baada ya hapo ni robo fainali.
MAZOEZI KUMTAFUTA MISS UKONGA YAENDELEA VIZURI
Mashindano ya kumtafuta Miss Ukonga 2012 kitongoji cha jijini Dar es Salaam, yanendelea kwa kasi katika Ukumbi maarufu Hiltec uliopo Ukonga, Banana, jijini Dar es Salaam ambapo warembo hao wanadai kila moja atakuwa mshindi katika shindano hilo.
Mazoezi hayo yalishuhudiwa na Miss Tanzania wa sasa, Salha Israel, na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga. ambao walitoa ushauri kadhaa kwa warembo hao.
Fainali ya mazoezi hayo itafanyika Mei 5 mwaka huu katika Ukumbi wa Wenge Guarden ulipo Ukonga FFU.
PICHA NA GPL
Subscribe to:
Posts (Atom)
































