Social Icons

Thursday, 15 October 2015

BONGO MUVI KUFANYA WHATSAPP GROUP PARTY

Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.
 Mratibu wa party hiyo, Abdul Ally ‘Mangi wa Vocha’ akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) kulia kwake ni mwakilishi wa Bongo Muvi, Vanessa Msofe, Kushoto ni mweka hazina wa party hiyo, Pinnar Sangawe. Waliosimama kuanzia kushoto ni Ismail Mussa mwakilishi wa TMT mwaka 2015, mwakilishi wa video Queen, Sophia Hassan, Mwakilishi wa Comedy, Sharo Mahela.

Mwakilishi wa Bongo Muvi, Vanessa Msofe akifafanua jambo.

Wasanii wa filamu Bongo wanaounda kundi la mtandao wa kijamii la whatsapp linalojulikana kwa jina la Bongo Talent Swahili wameandaa sherehe ya kundi lao linalowajumuisha wasanii mbalimbali wa maigizo ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 17 mwaka huu katika Hoteli ya KD iliyopo Kijitonyama jijini Dar.

Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa sherehe hiyo, Abdul Ally ‘Mangi wa Vocha’ alisema kuwa sherehe hiyo itahudhuriwa na wageni waalikwa ambao ni mastaa wakubwa wa Bongo muvi, ambao ni Baga Mteme, Faridi Uwezo, John Kallage na wengine kibao.

Naye mwakilishi wa Bongo Muvi, Vanessa Msofe alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani za aina mbalimbali, chakula na vinywaji huku suala la muhimu kabisa likiwa ni kubadilishana mawazo kuhusu mwenendo wa tasnia nzima ya filamu nchini na kuongeza kuwa party hiyo itaingia hadi mikoani na kuanzia na jiji la Mwanza ambalo litajumuisha wasanii wa filamu nchini humo.

No comments: