Social Icons

Wednesday 21 October 2015

BREAKING NEWS: MASHA AFIKISHWA KIZIMBANI CHINI YA ULINZI MKALI‏ WA POLISI

Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.

Laulensi Masha akiwa na wakili wake Elias Kifunda wakiwa wanabadilishana  mawazo  kabla ya kusomewa mashitaka yaliyokuwa  yakimkabili ya kufanya  mkutano bila kibali na kuingia kwenye makazi ya wakimbizi bila kibali
 Laulensi Masha akiwa na watuhiwa wenzake wakiwa wamefikishwa katika Mahakama  ya  Wilaya ya Mpanda kijibu tuhuma zilizokuwa zikiwakabili za kufanya mkutano bila kibali na kuingia kwenye  makazi ya wakimbizi bila kibali   
Picha na Walter  Mguluchuma wa Katavi yetu Blog


Na Walter Nguluchuma-Blogs za Mikoa
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Laulensi Masha akiwa na viongozi  sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA) wa Mkoa wa Katavi wamefikishwa katika  Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kufanya mkutano wa hadhara  na kuingia bila kibali kwenye Makazi ya Wakimbizi ya  Katumba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  huku wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi waliokuwa na Bunduki na mabomu ya machozi
Masha na  watuhumiwa  wenzake sita walifikishwa kizimbani jana  mbele ya Hakimu Mkazi  Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa na kusomewa  mashitaka na mwanasheria wa kutoka ofisi ya mwanasheria ya Mkoa wa Katavi  Lungano  Mwasubila
 Watuhumiwa waliosomewa mashita na mwanasheria wa Serikali ni Laulensi Masha, Gerald Kitabu  mgombea  Ubunge wa Jimbo la Nsimbo(CHADEMA) Abrahamu Mapunda mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mpanda,Fransico Misigalo  katibu wa  bavicha  wa Mkoa wa Katavi , Sinsilausi  Kaswele Mwenyekiti Chadema wa jimbo la Nsimbo  Lameck  Costantino  Katibu wa Chadema jimbo la Nsimbo na  Galus Adamu  mwanachama wa Chadema
Mwanasheria wa Serikali  Lugano  Mwasubila alidai mahakama hapo kuwa Masha ambae ni mtuhumiwa wa kwanza walitenda kosa hilo hapo  oktoba 19 mwaka huu majira ya saaa saba mchana huko katika Makambi ya Wakimbizi ya Katumba
Watuhumiwa wanadaiwa walisomewa mashitaka matatu ambapo   kosa la kwanza wameshitakiwa kwa kuingia kwenye makazi ya wakimbizi bila kibali cha Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi
Shitaka la pili wameshitakiwa kwa kosa la kufanya mkutano kwenye makazi ya wakimbizi ya katumba na shitaka la tatu wameshitakiwa kwa kosa la kuingia kwenye kambi ya wakimbizi wa Katumba bila kibali cha Mkuu wa Makazi ya wakimbizi ya Katumba
Hakimu Chiganga baada ya watuhumiwa kusomewa mashitaka hayo na mwanasheria wa Serikali aliwataka watuhumiwa  wajibu mashitaka hayo   na watuhumiwa wote saba walikana mashitaka hayo
Baada ya  Masha na watumiwa  wenzeke  saba kukana  mashitaka  hayo mwanasheria wa Serikali   Mwasubila aliiomba Mahakama isitowe mdhamana kwa Laulensi Masha  kwa kile alichodai mahakamani hapo kuwa Masha anakesi nyingine ya jinai katika Makakama  ya Kisutu Dares salaam  hivyo hatakiwi kupewa dhamana   ila watumiwa wengine sita wao dhamana zao zipo wazi
Mwanasheria aliyekuwa akiwatetea  Masha na wenzake Elias Kifunda alipinga pingamizi hilo kwa kile alieleza kuwa  Masha alifikishwa Mahakamani  Kisutu  lakini    Mahakama  bado haija mtia hatiani  hivyo  anayo haki ya kupewa mdhama endapo  kama itatimiza mashariti
Baada ya mabishano ya kisheria baina ya Mwanasheria wa Serikali  na wakili Kifunda  yaliodumu kwa dakika 30 Hakimu  Chiganga alilazimika kuharisha kesi hiyo kwa muda wa dakika 40 ili  kupitia  vifungu vya  sheria walivyokuwa wakibishania wanasheria hao ili aweze kutowa maamuzi ya kukubali mdhamana wa Masha au kukataa
Hakimu Chiganga baada ya kupitia vifungu vya sheria  alikubaliana  na   ombi la    Wakili wa Masha la kupewa mdhamana Laulensi Masha kwa kile aliileza  Mahakama kuwa  shitaka aliloshitakiwa nalo Mahakama ya Kisutu alimfanyi MashaMahakama imnyime adhabu kwa kile alieleza kuwa bado shitaka alinalo alijamtia hatiani
Hivyo  Mahakama  iliwapatia mdhamana  Masha na wenzake sita kwa mashariti ya kudhaminiwa na mtu mmoja  kwa kila mtuhumiwa kwa kiasi cha shilingi laki moja kwa kila mtuhumiwa na watuhiwa wote walitimiza mashariti  na  kuachiwa
Hakimu  Mkazi  Chiganga Ntengwa baada ya watumiwa kutimiza mashariti alihairisha kesi hiyo  hadi Nombe 19 mwaka huu

Na katavi yetu Blog (Blogs za Mikoa)


No comments: