Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.
Aliyekuwa Mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM, Deogratias Filikunjombe, enzi za uhai wake akipanda chopa yake.
Nakupenda Deo
Nimesikitishwa
sana na kifo chako. Kweli kifo kipo na kila mmoja wetu atakipitia
lakini cha aina hii, cha kijana aliyekuwa akipigania watu wake kiasi
hiki? Kinaumiza sana, hata hivyo, hatuna budi zaidi ya kukubali kuwa Deo
Filikunjombe, jembe la mkono limeondoka.
Chopa iliyosababsha kifo cha Filikunjombe, Capt. William Silaa na watu wengine wawili.
Nasema
kutoka ndani ya moyo wangu, taifa limepoteza mtu muhimu sana, hakusita
kupigania alichokiamini bila uoga wala hofu! Wakati mwingine
alitofautiana na msimamo wa chama chake kwa maslahi ya Watanzania
maskini, kwako ukweli ulikuwa nguzo. Nenda Deo, nenda kapumzike muda si
mrefu tutaungana nawe, kila mwanadamu atafariki dunia maana ndivyo
ilivyoandikwa.
Lakini
cha muhimu ni mtu atakuwa anafanya nini wakati anakufa! Je, atakuwa
akiiba au akifanya uzinzi? Deo umekufa ukitumikia watu wako, umekufa
kifo chema na Wanaludewa watakuombea. Nenda Deo, pumzika Deo, mema yako
yamekutangulia.
Hayo
ndyo yatakutetea mbele ya Maulana! Mwisho nasema kwa uchungu na
ninakuahidi, pale ulipoishia, sisi tutaendelea bila kujali tupata nini
mpaka siku moja wananchi wa taifa hili wafaidi mema ya nchi yao.
Nenda
Deo, kapumzike kwa amani, umekufa katika mapambano. Natoa pole kwa
familia yako, mkeo, watoto, wazazi na wananchi wote wa Jimbo la Ludewa,
msiumie sana, Mungu anajua ni kwa nini ameamua jambo hili litokee.
Naamini Deo yuko mahali sahihi, kutokana na kile alichokuwa akikifanya
wakati anakutwa na mauti, kwetu sisi, kibinadamu ni maumivu lakini
kiimani, Deo yuko mahali salama. Nenda kaka Deo. Pumzika kwa amani kaka!
Eric James Shigongo,
Eric James Shigongo,
Mkurugenzi, Global Publishers Ltd.
Nenda kamanda wangu Deo
Nenda kamanda wangu Deo
No comments:
Post a Comment