Social Icons

Thursday, 22 October 2015

LEO KATIKA MAHUSIANO: UNAINGILIA NDOA YA MWANAO UNATAKA AKUOE WEWE? HII NI SEHEMU YA PILI , INGIA HAPA UELEWE ISIJE IKAWA ANAINGILIA BILA WEWE KUJUA.

Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.

Bila shaka yoyote mmeamka mkiwa na afya njema na mnaendelea vizuri sana katika ujenzi wa taifa letu. Baada ya hayo, tuendelee na mada yetu ambapo wiki hii tutaendelea na sehemu ya pili inayowahusu wakwe wanaopenda kuingilia ndoa za watoto wao ambapo wiki iliyopita tuliishia katika kipengele kinachohusiana na mtoto wako akishindwa kuoa si utamaliza waganga?

Moja kwa moja utakuwa una maana kuwa hutaki mkwe, wamama wakwe wenye gubu ni bora ukamuacha mwanao akakaa kwake na wewe kwako kuliko kwenda kumfukuzisha mkweo kwani kama ulikuwa hutaki aoe basi naweza kudiriki kusema wewe ndiyo unataka akuoe kitu ambacho hakijawahi kutokea ulimwenguni na hakiwezi kutokea kwani nafasi ya mama itabaki kuwa ya mama tu.
Makabila yanachangia
Kwa makabila mengine kwao wanaona ni sawa mama kuingia kwenye chumba anacholala na mke wake lakini mengine ni mwiko kabisa kujua mkweo analala vipi kwa sababu ipo siku utamjua yukoje kupitia chumba chake na hapo ndiyo chokochoko zitakapoanzia.
Hebu fikiria eti mama mkwe ikifika asubuhi anakwenda kugonga mlangoni kwa mkwewe mbona hamuamkii, leo hatunywi chai, kwani huna aibu wewe? Je, kama wako faragha kwa muda huo? Huenda ndiyo wanatafuta wajukuu.
Mama mkwe mwache mkweo huru
Kwa wale mama wakwe mnaopenda kuwafuatilia wakwe na kuingilia mambo ya nyumbani kwao nawasihi sana muache wawe huru kwani hata wewe uliwahi kuwa na ndoa yako au bado una ndoa yako hakuna anayekuingilia sasa ni kwa nini umkoseshe amani mkweo mpaka atamani kuhama nyumba wewe unapopiga hodi?
Kwa wamama 
wakwe wote
Kumbuka malipo ni hapahapa duniani kama unamtenda wa mwenzako hata wako atatendwa tu, mpe nafasi ya kufurahia ndoa yake, wapo wanaowahesabia wakwe zao mpaka siku ya kushika ujauzito mwingine hii si kazi yako kwanza ni kazi ya Mungu, pili ni kazi ya yeye mwenyewe anayebeba ujauzito.
Nimelichomeka hili kwa sababu wapo mama wakwe wanaowabeza hata wakwe zao wasiozaa, utasikia wenzangu wana wajukuu mimi ndiyo sina, si suala zuri kulalamika muachie Mungu kwani ndiye muweza wa yote.
 Na GPL

Tafadhali usikose Uhondo huu zaidi.....

No comments: