Social Icons

Wednesday 21 October 2015

LOWASSA AONGOZA MAMIA KUUAGA MWILI WA DK.EMMANUEL MAKAIDI VIWANJA VYA KARIMJEE DAR ES SALAAM

Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, Dk. Emmanuel Makaidi wakati wa ibada ya kuuaga iliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam leo mchana. Katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali walihudhuria.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wananchi wakiwa wamejipanga foleni wakati wakienda kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula (kulia), akipeana mkono wa pole na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakati alipofika kuhudhuria ibada hiyo.

Mjane wa marehemu, Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela akiwa ameinua mikono wakati akimuaga mumewe katika ibada hiyo
Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mtungi, akizungumza kwa niaba ya serikali wakati wa misa hiyo ya kumuaga Dk. Makaidi.

Lowassa na Sumaye wakiteta jambo katika ibada hiyo.
Mchungaji David David (kulia), akiongoza ibada hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (katikati), akiwa na viongozi wengine katika ibada hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua matukio ya ibada hiyo.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa (wa pili kulia), akiwa na viongozi wa Ukawa. Kulia ni Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Waombolezaji wakiwa wamejipanga foleni wakati wa kwenda kutoa heshima za mwisho.
Ibada ikiendelea.
Ndugu jamaa na marafiki wakiendelea na kumuaga Dk. Makaidi.

Ni vilio na huzuni baada ya ibada hiyo ya kumuaga mpendwa wetu Dk. Makaidi.
Jeneza lenye mwili wa Dk. Makaidi likiingizwa kwenye gari tayari kuelekea makaburi ya Sinza kwa mazishi.

Na Dotto Mwaibale

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Profesa Mwesiga Baregu amesema kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democratic (NLD), na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dk. Emmanuel Makaidi ni kiashiria tosha cha ushindi wa umoja huo.

Mwenyekiti huyo mwenza wa Ukawa, amezikwa leo jioni  katika makaburi ya Sinza jijini hapa, huku yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.

Profesa Baregu aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akitoa salamu za rambirambi na kwa wanafamilia, wanandugu, wanachama na wanasiasa mbalimbali nchini walioguswa na kifo hicho wakati ibada fupi kutoa heshima za mwisho Dk.Emanuel Makaidi yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee.

"Tutaendelea kumkumbuka hususani pale ilipokundwa Ukawa kwani alikuwa miongoni mwa wabunge waliodiriki kususia bunge la katiba lililokuwa likiendelea," alisema.

Alisema kuwa kwa sasa nguvu ya Ukawa inaonekana kukuwa waziwazi na kifo chake kina ashiria kwamba katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika 25 mwezi huu umoja huo utashinda.

Msajili wa vyama vya siasa.

Kwa upande wake Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi alisema kifo hicho kimeacha pengo kubwa kwani alikuwa mkereketwa wa mabadiliko katika siasa.

Makamu Mwenyekiti NLD.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti NLD, Mfaume Hamisi, alisema kuwa chama hicho kitaendelea kiukumbuka na kuyasimamia misimamo na mambo aliyoyaamini Dk.Makaidi wakati wa uhai wake.

Mbatia.

Akizungumza kwa niaba ya Ukawa, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, James Mbatia alisema umoja huo utaendelea kumuenzi Dk.Makaidi na kubainisha kuwa alikuwa akiamini mageuzi na mabadiliko nchini lakini hadi leo hawako nae tena.

Msemaji wa Familia.

Kwa upande wake Oscar Makaidi ambaye ni msemaji wa familia ya marehemu aliutaka umoja huo kuendelea na kazi katika siku hizi chache zilizobaki kuelekea katika uchaguzi mkuu na kuongeza ushirikiano katika chama hicho kwani aliyekufa ni Makaidi na si chama.

Mangula.


Akitoa salamu za pole na rambi rambi, Makamu Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula alitoa pole kwa wanafamilia wanasiasa kwa kuondokewa nzao.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments: