Social Icons

Tuesday 20 October 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA KITUO CHA MICHEZO KIDONGO CHEKUNDU

Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kituo cha michezo cha Jakaya M.Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba mtoto wakati wa Sherehe za ufunguzi wa kituo cha michezo cha Jakaya M.Kikwete Youth park huko kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha michezo  cha Jakaya M.Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kimejengwa kwa msaada wa klabu ya michezo ya Sunderland ya Uingereza kwa kushirikiana na kampuni ya kufua umeme ya Symbion.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe  katika ufunguzi wa Kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akicheza mpira na baadhi ya watoto wanaopata mafunzo ya michezo katika kituo hicho kinachofunza mpira wa miguu,kikapu na volleyball ya ufukweni.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaopata mafunzo katika kituo kipya cha michezo.



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Symbion Bwana Paul Hinks baada ya sherehe za ufunguzi wa kituo(picha zote na Freddy Maro)

No comments: