Social Icons

Monday 12 October 2015

Waziri Magembe azindua bodi ya DAWASA, aitaka ichape kazi

Ikiwa una Tukiko lolote au Habari yoyote usisite kutumia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Profesa Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Saalam (DAWASA)jijini Arusha, katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jiji la Arusha(AUWSA) Felix Mrema na Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba.
Katibu Mkuu wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Mfutakamba akizungumza wakati wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Saalam (DAWASA) jijini Arusha.
3
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akijadilia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Majisafi na Usafi wa Mazingirajiji la Arusha (AUWSA), Felix Mrema (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira, Mhandisi Ruth Koya wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Saalam(DAWASA) jijini Arusha.
WAZIRI wa Maji,Profesa Jumanne Maghembe  amezindua Bodi  mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa) na kuitaka kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii katika mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi.
Maghembe alitoa kauli hiyo  jijini Arusha na kusema kuwa serikali imepata kiasi cha dola za Marekani 409 kutoka Benki ya Dunia,Korea Kusini na wadau wengine kuweka miundombinu ya majitaka itakayosaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira kwenye bahari ya Hindi.
Alisema idadi ya watu katika jiji la Dar es Salaam inaongezeka kila mara hiyo serikali imejipanga kuhakikisha inatengeneza miundombinu itakayowezesha upatikanaji wa maji safi na maji taka unaondana na hadhi ya jiji.
“Benki ya Dunia imetoa kiasi cha dola 220 milioni na Serikali ya Korea ya Kusini dola 89 milioni ambazo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kukabiliana na changamoto ya mahitaji ya maji na uboreshaji miundombinu ya Maji taka,”alisema Profesa Maghembe
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba alisema kumekua na maboresho makubwa baada ya kuchimbwa visima virefu kwenye maeneo ya Kimbiji  na Mpera hatua ambayo imewapa wananchi maji kwa kiwango cha kuridhisha kufikia asilimia 68 ya mahitaji.
Mwenyeketi wa Bodi ya Wakurugenzi (Dawasa)Dk. Eve Sinare alisema watashirikiana na Menejimenti  kukabiliana na  changamoto za maji kwa kushirikiana Dawasco na wadau wengine.
Alisema katika kipindi kilichopita bodi yake ilipata mafanikio kutokana na kutokuingilia Menejimenti katika utendaji kazi kwani sio jukumu la bodi kuingilia utendaji wa Dawasa wa siku kwa siku.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo ni  Dk Eve Hawa Sinare,Makamu mwenyekiti wake ni  Meja Jenerali Samueli Kitundu ambaye ni Mwenyekiti wa Dawasco huku wajumbe wengine ni  Paul Sulley, Mhandisi Peter Chisawillo, Profesa Felix Mtalo,Lason Msongolena, Archard Mutalemwa, Abbas Mtemvu, Abdalah Bulembo,Mgeni Baruani na Dk James Wanyancha.

No comments: