Social Icons

Monday 12 May 2014

LEO KATIKA MAHUSIANO: UKICHEPUKA MARA MOJA, INAWEZA KUYAGHARIMU MAISHA YAKO YOTE , SOMA HAPA KWA MAKINI

Tukiendelea na mada yetu kutoka pale tulipoishia wiki iliyopita, suala la kuchepuka ni la kupiga vita. Anayekuja kwako na vishawishi vya hapa na pale ndiye adui yako pale mambo yanapogeuka. Ukichepuka utamuumiza sana mwenzio, kisha nawe utaumia.

Hii ni kwa sababu mateso ya mwenzi wako hayawezi kukupa ahueni. Kwa walio kwenye mapenzi ya dhati ni kwamba mwenzi wako anapoteseka, na wewe pia unakuwa kwenye mateso makali. Maana furaha yake ni yako, maumivu yake yanakugusa pia. Vivyo hivyo kilichopo kwako naye kinamhusu kwa tafsiri pana.

Juu ya hapo ni kuwa hisia za maumivu katika mapenzi zina kawaida ya kuhama kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Unamtesa sana, siku akichukua uamuzi wa kusema “mwana kwenu kwa heri”, hapo ndipo unashtuka, eti huamini kinachotokea.

Maombi ya msamaha kutoka kwako kwenda kwake yanakuwa kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana. Kwa nini mfike huko? Akili yako itumikishe kufanya uamuzi sahihi ambao ni kumtunza mwenzi wako ambaye anakutunza hivi sasa. Maudhi ya hapa na pale jiepushe nayo.

Mdharau mwiba guu huota tende! Usione anachokilalamikia mwenzi wako ni kidogo, mfanye afurahie uwepo wako kila siku. Usimruhusu akulilie, maana ipo siku utalia wewe. Hakikisha hatoi machozi ya maumivu, isipokuwa yawe ya furaha. Kinyume chake kuna siku yatakugeuka.

ASIMULIAYE MVUA IMEMNYESHEA
Maryam Zambi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 46. Ni mama wa watoto wanne, yupo kwenye ndoa kwa mwaka wa 19 sasa. Aliolewa na Raphael Zambi, 51, mwaka 1995. Akiwa na watoto wawili, aligundulika kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.

Mume wake, aligundua ukaribu usiofaa kati ya Maryam ‘Mama Dennis’ na dereva taksi aitwaye Sospeter. Akafuatilia na kubaini kwamba upo uhusiano wa kimapenzi kati yao. Raphael ‘Baba Dennis’, aliumia sana, kwani kabla ya hapo alikuwa akimwamini mkewe kwa kiwango kikubwa sana.

Mama Dennis anasimulia: “Mume wangu ni mzuri, anajali, ni baba mzuri wa familia. Kipaumbele chake siku zote ni familia yake. Kwa jambo lolote lile, huwa ananiweka mbele hata ya ndugu zake. Hajawahi kunifanyia kitendo cha kuniumiza wala kunisaliti.

“Huko nyuma hatukuwa na magari, kwa kawaida mume wangu alifuatwa asubuhi kwenda kazini na gari la ofisini kwake, kwa hiyo alichofanya ikawa lile gari la kazini kwa mume wangu ndilo lililonipeleka ofisini kwangu kila siku asubuhi, baada ya hapo ndipo mume wangu alielekea sehemu yake ya kazi.
“Kwa maana hiyo, nilipata lifti ya gari la kazini kwa mume wangu kila asubuhi na wakati wa kutoka, siku nyingine alinipitia na kurudi nyumbani pamoja na pale alipokuwa na ratiba nyingi za kiofisi kiasi cha kumfanya achelewe kurudi nyumbani, alinipa fedha ya taksi.

“Mume wangu hakutaka nipande daladala, alikuwa na upendo mkubwa sana. Sijui kwa sababu ya upofu au kiburi cha kuona napendwa, mimi sikumpa mume wangu upendo ambao alistahili kulingana na ukweli halisi wa jinsi alivyokuwa ananijali.

“Basi ikawa wakati wa kutoka kazini kama mume wangu hanipitii turudi wote nyumbani, napanda taksi. Ni usafiri huo ndio ukanikutanisha na dereva taksi anayeitwa Sospeter ambaye nilizoea kumwita Sos kutokana na mazoea niliyokuta kwamba madereva wenzake walizoea kufupisha jina lake na kumwita hivyo.

“Sos akawa ndiye dereva niliyemwamini na tukazoeana. Wala Sos hakunitongoza, yalianza mazoea ya utani wa hapa na pale, tukiwa njiani mara nimpige singi, wakati mwingine kofi, naye akawa anarudisha hivyohivyo. Kweli mzahamzaha mwisho hutunga usaha!

“Siku moja sijui nini kilitokea, katika utani na michezo ya hapa na pale, nilishangaa Sos kasimamisha gari na kulipaki pembeni ya barabara kisha tukaanza kunyonyana ndimi. Gari la Sos lina vioo vya giza (tinted) na hilo ndilo lilitupa jeuri ya kufanya hicho kitendo kwa muda mrefu sana.

“Hatukuishia kunyonyana ndimi peke yake, tulishikana maeneo tofauti, kwa kifupi tulichokifanya kwenye gari siku hiyo, kilikuwa ni ‘romansi’ tosha. Baadaye ilikuwa kama vile nimeshtuliwa, nikamsukuma Sos, nilipojiangalia dah! Niliona aibu sana.

“Tayari Sos alikuwa ameshanifungua zipu na ile stara ya kifuani alikuwa ameshaiondoa, kwa hiyo aliweza kuchezea vitikiti maji vyangu viwili vya pale kifuani kwa kadiri alivyotaka. Kuna nyakati pia alipandisha juu sketi niliyokuwa nimevaa, akawa anafanya utalii kwenye mapaja yangu.

“Kimsingi Sos aliutawala mwili wangu utadhani yeye ndiye mume wangu. Zaidi huwa nafikiria kuwa kila kilichofanyika hakikuwa heshima kwa sababu mume wangu asingeweza kunifanyia yale ambayo Sos alinifanyia pembeni ya barabara ndani ya gari. Mume wangu ananiheshimu na anapenda faragha.

“Nilijutia kwa kiasi fulani, nikawa nimejiinamia pale kwenye kiti. Sos hakunipa muda niendelee kujuta, alinivutia tena upande wake, kipindi hicho nilikuwa bado sijafunga zipu, kwa hiyo akapeleka mkono wake wa kulia kifuani kwangu, akaanza kuchezea tikiti maji langu la kushoto.

“Shetani ana nguvu sana, maana wakati Sos anafanya hivyo wala sikumzuia, nilikuwa mpole utadhani mbwa mbele ya chatu. Akanivutia tena kwenye midomo yake, kwa mara nyingine tukanyonyana ndimi. Siku hiyohiyo tulifika mbali sana kimahaba lakini hatukukamilisha safari yote ya mapenzi.”

Itaendelea wiki ijayo.


GPL

No comments: