Social Icons

Featured Posts

Friday, 20 October 2017

MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAPAZA SAUTI KIMATAIFA


Mratibu wa kampeni ya kuwezesha wanawake kutoka Oxfam Bi.Magdalena Thomas akielezea kwa ufupi hali ilivyo katika suala zima la kuwawezesha wanawake linavyohitaji nguvu zaidi huku akitolea mfano namna Mama Shujaa wa Chakula ilivyofanikiwa kuleta mtazamo chanya na kufumbua macho washiriki pamoja na jamii inayowazunguka.

Monday, 9 October 2017

TANZANIA KUSHIRIKI TAMASHA LA 19 LA DUNIA LA VIJANA NA WANAFUNZI Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Erick Shitindi akizungumza na baadhi ya vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la Vijana na Wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi kabla ya kuwakabidhi bendera mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

IHEMBE MABINGWA KOMBE LA MBUNGE WA KARAGWE

 Mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimpokea mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba

SHIELD OUR WATOTO'S FAMILY PICNIC & COOKOUT EVENT YAFANA WESTERVILLE, OHIO

Nyuku vikiwa vipo tayari kwenye picnic ya familia na nyama choma iliyoandaliwa na Shield Our Watoto siku ya Jumamosi Oktoba 7, 2017 Westerville, Ohio. SOW ni oganaizesheni iliyoanzishwa na Bhoke Kirigiti akishirikiana na mumewe PeterKirigiti inayotetea watoto kutokana na unyanyasaji hasa watoto wa kike inapowapigania hasa unyanyasaji wa kingono chini ya umri mdogo. Oganaizesheni hii hushirikiana na wazazi wa watoto na watu mbalimbali wakiwemo watoa elimu ya unyanyaswaji wa watoto wakishirikiana na mashirika mbalimbali yasiyokua ya Kiserikali. Shield Our Watoto hutoa elimu ya bure kwa wazazi na watoto kuhusiana na unyanyasaji  wa kijinsia wanaofanyiwa watoto wenye umri ndogo ambao kati ya watoto 3 kati ya 10 wamekua wakiathirika kisaikolojia kutokana unyanyasaji huo

Sunday, 8 October 2017

KAMPUNI YA BIMA YA RESOLUTION YAZINDUA NJIA YA IRAP ILI KUWAJENGEA UWEZO WAFANYAKAZI WAKE,JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati akielezea mabadiliko mbalimbali ya kampuni,katika utendaji kazi na kuwajibika kwa wafanyakazi na kuwasisitiza kuchapa kazi zaidi.

Thursday, 5 October 2017

UNESCO, ILO, UNICEF, UNDP NA EDUCATION INTERNATIONAL YATOA SALAMU KWA WALIMU DUNIANI


Kufundisha Kwa Uhuru, Kuwawezesha Walimu
Walimu ni msingi mkuu katika ustawi wa muda mrefu wa kila jamii kwa kuwa hujishughulisha kuwapatia watoto, vijana na watu wazima elimu na ujuzi wanaohitaji ili kufikia uwezo wao.
Lakini duniani kote, walimu wengi sana hawana uhuru na msaada wanaohitaji kufanya kazi yao iliyo muhimu sana. Ndiyo maana maudhui ya Siku ya Walimu Duniani kwa mwaka huu – ‘'Kufundisha kwa Uhuru, Kuwawezesha Walimu'’ - inathibitisha thamani ya walimu waliowezeshwa na kutambua changamoto ambazo wengi hukabiliana nazo katika maisha yao ya kitaaluma ulimwenguni kote.
Kuwa mwalimu aliyewezeshwa ina maana ya kuwa na uwezo wa kupata mafunzo yenye ubora, malipo ya haki, na fursa zisizo na mwisho za kujiendeleza kitaaluma. Pia inamaanisha kuwa na uhuru wa kuunga mkono maendeleo ya mitaala kitaifa – na uhuru wa kitaaluma wa kuchagua njia sahihi na mbinu zinazofaa zaidi kuwezesha utoaji wa elimu yenye ufanisi, jumuishi na ya usawa. Zaidi ya hayo, inamaanisha kuwa na uwezo wa kufundisha kwa usalama wakati wa mabadiliko ya kisiasa, machafuko, na migogoro.
Lakini katika nchi nyingi, uhuru wa kitaaluma na uhuru wa mwalimu viko chini ya shinikizo. Kwa mfano, katika ngazi za shule za msingi na za sekondari katika baadhi ya nchi, mipango ya uwajibikaji imeweka shinikizo kubwa kwa shule kutoa matokeo kwa vipimo vilivyowekwa, na kupuuza haja ya kuhakikisha mtaala wa msingi unaofaa mahitaji tofauti tofauti ya wanafunzi.
Uhuru wa kitaaluma ni muhimu kwa walimu katika kila ngazi ya elimu, lakini ni muhimu zaidi kwa walimu wa elimu ya juu, ili uwawezeshe kutumi uwezo wao wa kuvumbua, kuchunguza, na kuendeleza utafiti kuhusiana na namnaza kisasa zaidi za kufundisha. Katika ngazi ya elimu ya juu, mara nyingi walimu hupatiwa mikataba ya ajira ya kipindi maalumu. Hii inaweza kusababisha hali ya kutokuwa na uhakika wa ajira kwa walimu, kupungua kwa matarajio ya kukua kitaaluma, mzigo mkubwa wa kazi na malipo duni – yote haya yanaweza kuzuia uhuru wa kitaaluma na kudhoofisha ubora wa elimu ambayo walimu wanaweza kutoa.
Katika ngazi zote za elimu, shinikizo la kisiasa na maslahi ya kibiashara yanaweza kuzuia uwezo wa walimu kufundisha kwa uhuru. Waalimu wanaoishi na kufanya kazi katika nchi na jamii zilizoathiriwa na migogoro na machafuko mara nyingi hukabiliwa na changamoto kubwa zaidi, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa kuvumiliana, ubaguzi, na vikwazo vinavyohusiana na utafiti na kufundisha.
Mwaka huu unaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Mapendekezo ya UNESCO ya 1997 kuhusu Hali ya Wakufunzi wa Elimu ya Juu, ambayo inakamilisha Mapendekezo ya UNESCO / ILO ya 1966 kuhusu Hali ya Walimu. Kwa pamoja, vyombo hivi hufanya mfumo mkuu wa rejea juu ya haki na wajibu wa walimu na waelimishaji. Yote yanasisitiza umuhimu wa uhuru wa mwalimu na uhuru wa kitaaluma katika kujenga ulimwengu ambapo elimu na kujifunza ni kwa ajili ya wote.
Wakati dunia inapofanya kazi pamoja ili kufikia maono ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, tunawaomba washirika wetu katika serikali, sekta ya elimu na sekta binafsi kujitolea kubeba jukumu la kuwaandaa waelimishaji wenye ujuzi ulio bora zaidi, wenye thamani na waliowezeshwa. Hii ni njia muhimu katika kuyafikia maono ya Malengo ya Maendeleo Endelevu hasa lengo namba 4 lenye nia ya kuwa na ulimwengu ambapo kila msichana, mvulana, mwanamke na mwanaume wanapata elimu bora na fursa za kujifunza katika maisha yao yote.
Hii inamaanisha kuwapatia walimu mazingira mazuri ya kazi na mishahara iliyo bora, ikiwa ni pamoja na walimu wa ngazi ya juu. Inamaanisha kuwapa walimu mafunzo na fursa ya kujiendeleza. Inamaanisha kuongeza idadi ya walimu wenye ubora, hasa katika nchi zenye idadi kubwa ya walimu na waelimishaji wasio na elimu ya kutosha. Inamaanisha ya kuondoa vikwazo visivyo vya lazima katika utafiti na kufundisha na kulinda uhuru wa kitaaluma katika ngazi zote za elimu. Na mwisho, inamaanisha kuinua hadhiya walimu duniani kote kwa namna ambayo inaheshimu na inayoonyesha matokeo waliyonayo walimu katika jamii.
Katika Siku hii ya Walimu Duniani, ungana nasi katika kuwawezesha walimu kufundisha kwa uhuru ili kwamba, kila mtoto na kila mtu mzima awe huru kujifunza – kwa manufaa ya dunia iliyo bora zaidi.
Imetolewa na Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO; Guy Ryder, Mkurugenzi Mkuu wa ILO; Anthony Lake, UNICEF Executive Director; Achim Steiner, UNDP Administrator; pamoja na Fred van Leeuwen, General Secretary of Education International.

Wednesday, 4 October 2017

BENKI YA UBA TANZANIA WAZIDI KUNG'ARA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA


 Afisa huduma kwa wateja wa Benki ya UBA Tanzania, Bi Stella Matau akifurahia kumuhudumia mmoja wa wateja wao wakubwa aliyefika katika benki hio huku benki hio ikiendelea kung'ara katika kutoa huduma bora kwa wateja kwa wakati wote

Tuesday, 3 October 2017

BENKI YA NMB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, YAAHIDI KUBORESHA HUDUMA


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker akizungumza katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika hafla iliyofanyika leo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

Wednesday, 27 September 2017

JUMIA TRAVEL YAUNGANA NA DUNIA KUADHIMISHA SIKU YA UTALIINa Jumia Travel Tanzania

Kila ifikapo Septemba 27 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya utalii duniani. Maadhimisho hayo hufanywa na kila nchi ambapo kunakuwepo na shughuli kadhaa zikiongozwa na malengo na kauli mbiu tofauti zilizoazimiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO).

UJUMBE WA MKURUGENZI MKUU WA UNESCO KATIKA SIKU YA KIMATAIFA YA UFIKIVU HABARI SEPT 28

Katika ulimwengu wa uchangamano, ufikivu wa habari ni muhimu katika kujenga jamii yenye maarifa, iliyo shirikishi na endelevu. Huu ndio ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote (IDUAI), ukizingatia jukumu muhimu ambalo ufukivu wa habari hufanya katika kuendeleza Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu. 

Tuesday, 26 September 2017

VODACOM SASA KAZI NI KWAKO YAJA NA PINDUA PINDUA UNITKatikati Mwenye Kofia Ni Mkurugenzi Wa Vodacom Tanzania Bw. Ian Ferrao Akiwa Na Timu Ya Vodacom Wakati Wakuzindua Pindua Pindua Units Mbele Ya Wafanyakazi Wa Vodacom Katika Ofisi Za Kampuni Hiyo Jijini Dar es salaam

KOLABO LA NANDY NA BETY G COKE STUDIO LAWA GUMZO

Baada ya onyesho la pili la Coke studio msimu wa tano kupitia luninga ya Clouds kuacha gumzo kwa washabiki wengi wa muziki,mwishoni mwa wiki katika onyesho la tatu walipagaishwa tena na kolabo za wasanii mbalimbali zenye midundo ya kiafrika na zilizosukwa kwa ustadi mkubwa na magwiji wa kutengeneza muziki .

Saturday, 23 September 2017

ECOBANK YAZINDUA NJIA SALAMA YA MALIPO KWA MTANDAO


 
  Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ,Ecobank Tanzania, Mwanaiba Mzee, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA .Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki  hiyo, Respige  Kimati  na Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja reja, Ndabu Sware (kushoto).

Friday, 22 September 2017

TCRA WAENDESHA WARSHA YA VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI NA KUZINDUA KAMPENI YA KUSISITIZA MATUMIZI BORA YA MITANNDAO YA KIJAMII.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jones Kilimbe akifungua rasmi warsha ya vyombo vya Habari Mtandaoni iliyo wahusisha Blogu na 'Online Tv' katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.