Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.
Kwanza
kabisa nianze kwa kusema kuwa mapenzi ni kitu kizuri kilichoumbwa kwa kila
kiumbe chenye jinsia.
Kwa wanadamu
mapenzi huwa ya kipekee zaidi kiasi kwamba kila mmoja amekuwa na tafsiri yake
lakini hakuna hata moja inayoweza kujikamilisha kuelezea kikamilifu kabisa
maana ya neno mapenzi japo kuwa katika nyakati tofautitofauti kila mtu
ameshawahi ‘ku-experience’ yaani kupitia mapenzi aidha kwa kupenda au kupendwa
au kupendana na mtu fulani.
Experience hiyo
ambayo kila mtu hupitia kwa kupenda au kupendwa huwa ni hisia nzuri ikiwa tu yule
unayempenda na yeye akakupenda na hatimaye mkawa penzini.
Hapo mtu
anaweza akajisikia yupo ulimwengu wa kipekee wenye furaha na raha zisizo na
kikomo na zisizoelezeka kwa maneno ya kawaida yenye herufi ‘a-z’.
Lakini hayo
yote yanaweza kugeuka na kuwa majuto na maumivu makubwa ikiwa tu mpenzi wako
akakusaliti au kukuacha wakati bado unampenda.
Hapo ndipo
utasikia kauli kama vile ‘mapenzi mabaya’ au ‘sitapenda tena’ zikianza na
kuwaogopesha wengine kuingia kwenye mapenzi tena kiasi kwamba wapo walioapa
kutopenda tena hata kama watu wenye mapenzi ya dhati wakitokea huwaacha wapite
bila kujua kuwa wanajikosesha bahati.
Ni wazi kuwa
hakuna maumivu makubwa zaidi kama yanayotokana na mapenzi lakini mapenzi
yenyewe siyo mabaya kiasi cha kugopwa bali ni mazuri sana kiasi kwamba kama
yakifuatwa kwa utaratibu sahihi unaweza ukaenjoi bila kuwa na majuto yoyote.
Wapi tunapokosea?
-Wengi tunakosea
kwa kupenda kuwa na wapenzi wazuri wa umbo, sura na hata sauti yaani kifupi
wanaovutia ili marafiki wakimtazama wamsifie. Hilo ndilo kosa la kwanza.
-Wengi tunapenda
kuwa na mpenzi ambaye anajiweza kifedha, suala linalochagizwa na maisha magumu
yaliyopo katika nchi nyingi za kiafrika hasa Tanzania ambapo mtu hushindwa kuwa
na mpenzi asiye na uwezo wa kifedha japo kuwa anampenda na kukimbilia kwenye
fedha ambapo hata hivyo huwa na penzi la upande mmoja yaani mmoja ndiye
anayempenda mwenzake kuliko mwenziye.
Lakini wakati
yote hayo yakifanyika Mungu kupitia zawadi hiyohiyo ya mapenzi aliyoitunuku
kwenye kile moyo ya mja wake, hubakia palepale ambapo bado kila mtu hujiona
mpweke au hajatimia kwa kuishi bila kuwa na penzi la dhati yaani bila kujisikia
kupendwa au kupenda.
Kikubwa ni
kwamba hata kama umeumizwa vipi na mapenzi bado mapenzi ya kweli yapo na kuna
mtu yupo ambaye anakutafuta wewe unayehitaji mapenzi ya dhati lakini hamjajuana
tu. Achana na kauli za ‘nimpendaye bado hajazaliwa,’ ukweli ni kwamba ameshazaliwa
kazi kwako.
Usikose kusoma
makala ya ijayo inayosema; MJUE MVULANA MWENYE MAPENZI YA DHATI KWAKO
itakayoletwa kwenu kupitia Darasa la Malovee hapahapa Fredy Njeje Blog. Kutoka
kwa Daktari wa Mapenzi. Contact: 0653146563.
Inaletwa kwenu na Fredy Njeje Blog
1 comment:
p
Post a Comment