Social Icons

Tuesday 22 November 2011

20%, Christina Shusho, Bonny Mwaitege, Glorious Singers Kuwasha Moto Street University Arusha







20%.
BONNY MWAITEGE.
Christine Shusho
Glorius Singer
--

Na mwandishi wetu
Wasanii wa muziki wa injili na kizazi kipya Bongo, Christina Shusho, Bonny Mwaitege, Abbas Hamis Kinzasa ‘20%’, Kundi la Waimbaji la Glorious Singer, Dot Com Generation na wengine wengi wanatarajiwa kuwasha moto wa burudani kwenye Tamasha la Street University litakalofanyika Novemba 27, mwaka huu jijini Arusha.


Tamasha hilo kubwa la ujasiriamali lenye kaulimbiu ya Kujikomboa na Kuondoa Umaskini kupitia Ujasiriamali litafanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo na kuwakutanisha wajasiriamali, wafanyabiashara na vijana watakaofundishwa mbinu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini kupitia ujasiriamali.


“Ukiachilia mbali burudani, tutatoa mafunzo ya ujasiriamali ikiwemo namna ya kupata wazo la kibiashara, kupata mbinu za kujitajirisha, kujifunza kuwa mwajiri badala ya mwajiriwa, jinsi ya kuomba mikopo mikubwa benki, kupanua mitaji na mada nyingine kemkem. Nawasihi watu wajitokeze kwa wingi kwani ni tamasha la kipekee kwa kiingilio cha Sh. 5000 tu,” alisema mratibu wa tamasha hilo, James Mwang’amba.


Watoa mada katika tamasha hilo ni wajasiriamali wa kimataifa na wazungumzaji wa kutia hamasa (motivational speakers) Eric Shigongo na Mwang’amba. Wadhamini wa tamasha hilo la kihistoria ni Kampuni ya Global Publishers Ltd, Malta Guiness, Airtel, Azania Bank na Mfuko wa Penseni ya Watumishi wa Umma (PSPF).


Wengine ni wauzaji na wasambazaji wa vipodozi asili wa Oriflame, Hoteli ya Corridor Springs ya Arusha, Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Wafanyabiashara na Wakulima (TCCIA), Hoteli ya Kibo Palace ya jijini Arusha, Tripple A Radio (88.5 FM), Sunrise Radio (94.8 FM), Mambo Jambo Radio (93.0 FM) na Radio 5 (105.7FM), zote za jijini humo.


No comments: