Social Icons

Thursday, 3 November 2011

ESKADO KUIBUKA NA WHAT’S YOUR FREEDOM KWENYE SWAHILI FASHION WEEK.



Na.Mwandishi wetu


Mbunifu anayekuja juu kwa kasi katika ubinifu wa mitindo ya nguo nchini, Doreen Estazia atazindua staili mpya ya viwalo ijulikanayo kwa jina la What’s Your Freedom (WYF) Novemba 11 katika tamasha la Swahili Fashion Week (SFW) lililopangwa kufanyika kwenye viwanja cha makumbusho ya Taifa jijini.


Estazia alisema jana kuwa ameamua kutoa staili hiyo kupitia lebo yake ya Estado Bird na viwalo hivyo ni moja ya kuadhimisha sherehe ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.


Alisema kuwa ameamua kubuni nguo hizo ili kutoa fursa kwa kila mvaaji awe huru na chaguo lake. Alisema kuwa nguo hizo zimetengenezwa malighafi ya hali ya juu na hali kadhalika ubora wake ni wa kipekee kabisa.


“Nimetengeneza nguo za jinsi zote tofauti na mawazo ya wengi, kuna nguo za kike za kila ana na vile vile kuna nguo za kiume, nataka kuonyesha kuwa nami ni miongoni mwa wabunifu bora katika fani hii,” alisema Estazia.


Alifafanua kuwa mbali ya kushiriki katika Swahili Fashion Week, pia amewaomba mashabiki wa masuala mavazi nchini kumpigia kura katika maonyesho hayo ya kila mwaka ili aweze kushinda katika kinyang’anyiro cha mbunifu anayekuja juu kwa kasi.


Alisema kuwa kula zinatakiwa kupigwa kwa kuandika lebo yake, Eskado Bird kwa mwaka 2011 kupitia mtandao, http://www.swahilifashionweek.com na vile vile kutembelea au kufungua mtandao wake, Eskado Bird fan katika Facebook au www.eskadobird.com kuweka ‘clip’.

No comments: