Social Icons

Thursday, 24 November 2011

FILAMU YA C.P.U KUANZA KUONESHWA RASMI IJUMAA TAREHE 25 NOVEMBA 2011 MLIMANI CITY CINEMAX CENTURY


Ile filamu ya C.P.U ambayo imekuwa ikisubiriwa na Watu wengi hatimaye mwisho wa wiki hii itaweza kuzinduliwa na kuoneshwa rasmi kwa wapenzi wa tasnia ya filamu.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa filamu ya C.P.U bwana Evans Bukuku alisema kuwa “Filamu ya C.P.U kwa mara ya kwanza itaoneshwa hapo Ijumaa tarehe 25 Novemba 2011 kuanzia saa 1 na dakika 45 jioni katika ukumbi wa Sinema wa mlimani city century cinemax, kisha itaendelea kuoneshwa kwa wiki nzima muda kama huo mpaka mnamo tarehe 1 Disemba 2011.
Hivyo basi hii itakuwa fursa pekee kwa wapenzi wa tasnia ya filamu na watanzania wote kwa ujumla kwenda kupata kujionea kazi ya ubora wa hali ya juu ambayo imefanyika hapa Tanzania.Kwa wale watakaopata nafasi ya kuitazama Filamu ya C.P.U hakika watathibitisha hili
Akizungumzia kwa ufupi juu ya Filamu hii Bw. Bukuku alisema, “ filamu ya C.P.U imetengenezwa na kampuni ya Haak neel kwa ushirikiano na Wegos Works Production ikiwa imeandikwa na Novatus Nago na kuongozwa na Karabani huku watayarishaji wakuu wakiwa ni Prof. Martin Muhando na Bw Godfrey Mahendeka. CPU ni aina ya hadithi ya kipelelezi yaani ‘Investigatory story’ ikiwa inazungumzia kitengo kilichoundwa kwa ajili ya kufuatilia na kutatua matatizo yanayowapata watoto.
Hivyo Maria Isabela (Sauda Simba) anateuliwa na serikali kuongoza timu hiyo, katika hilo inabidi awashawishi watakao msaidia ambao ni Alex Kibera(Nkwabi Juma) jambazi anayetumikia kifungo cha miaka 30 jela, David Kifati(steven Sandhu) mtaalamu wa kompyuta na kijana mwenye uelewa mkubwa ambaye anatoka katika familia bora na anayependa anasa, pia kuna Rehema Mlaki (Subira Wahure) akiigiza kama msichana anyefanya kazi ya uwakili wa kujitegemea.
Baada ya kufanikiwa kuwashawishi wanaanza kazi ya kwanza ambayo kiujumla ni yenye misukosuko na inayohitaji umakini wa hali ya juu kwa kuwa ni ya hatari sana hasa wanapokabiliana na mtu kama Jibaba(Mobby Mpambala) mmiliki wa danguro kubwa hapa jiji na mzoefu wa biashara haramu
hapo ndipo utapata kuona mikiki na ufanisi uliooneshwa na waagizaji takribani 180. Filamu ya CPU ikiwa imetengezwa hapa jijini Dar es Salaam katika maeneo tofauti zaidi ya 30.

No comments: