Social Icons

Tuesday, 8 November 2011

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) yafanya hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila la kheri wachezaji wa Taifa Stars dhidi yao na Chad


Pichani baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila kheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi yao na Chad,wakimsikiliza Waziri Mkuu,Mizengo Pinda kwenye Luninga kuhisiana na kuitakia kila la kheri timu ya Taifa,na kwamba katika kuifanikisha hilo ametoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo katika mambo yake mbalimbali,sambamba na hilo kupitia kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa timu hiyo,pia jioni ya leo walizindua kampeni ya tangazo la televisheni iitwayo TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA,hafla hiyo imefanyika kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa New Africa Hotel,jijini dar.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT),Dioniz Malinzi akimkabidhi bendera ya Taifa,Kapteni wa timu ya Taifa Stars,Henry Joseph pamoja na kocha wa timu hiyo,Jan Paulsen leo jioni kwenye hafla fupi ya kuagwa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Chad.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd,wakiongozwa na Mkurungezi wa Mawasiliano,Teddy Mapunda (wanne shoto), wakiwa katika picha ya pamoja jioni ya leo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila kheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi yao na Chad,sambamba na hafla hiyo SBL walizindua kampeni ya tangazo la televisheni iitwayo TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA,hafla hiyo imefanyika kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa New Africa Hotel,jijini dar.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT),Dioniz Malinzi akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa,Taifa Stars kwenye hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila kheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi yao na Chad,sambamba na hafla hiyo kampuni ya SBL walizindua kampeni ya tangazo la televisheni iitwayo TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA kwa ajili ya kuihamasisha jamii kuishangilia timu yao ishinde,hafla hiyo imefanyika kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa New Africa Hotel,jijini dar.


Rais wa TFF,Leodga Tenga akizungumza machache jioni ya leo kwenye hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila kheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi yao na Chad,sambamba na hafla hiyo kampuni ya SBL wamezindua kampeni ya tangazo la televisheni iitwayo TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA kwa ajili ya kuihamasisha jamii kuishangilia timu yao ishinde,hafla hiyo imefanyika kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa New Africa Hotel,jijini dar.


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL,Teddy Mapunda akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali jioni ya leo kwenye hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila lakheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi yao na Chad,ambapo pamoja na hilo SBL wamezindua kampeni ya tangazo la televisheni iitwayo TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA,kwa ajili ya kuihamasisha jamii kuishangilia timu yao iibuke na ushindi.Aidha Teddy amewashukuru Watanzania wapenda michezo kwa mshikamano walionao kwa timu yao ya taifa,kama vile haitoshi Teddy pia ameipongeza Serikali kwa mchango wake thabiti kwa timu ya Taifa na shauku ya kuona timu hiyo inafika mbali katika kampeni yake ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la Dunia huko Brazil ifikapo mwaka 2014,hivyo kuondokana na kasumba ya kuonekana kichwa cha mwendawazimu.

Bendi ya Muziki wa dansi, Kalunde band ikiongozwa na Deo Mwanambilimbi a.k.a Mzee Goba (pichani nyekundu) wakitumbuiza jioni ya leo kwenye hafla hiyo.









Kapteni wa timu ya Taifa,Henry Joseph akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Serengeti Breweries,mara baada ya kuzungumza machache mbele ya wageni waalikwa kuhusiana na mchezo dhidi yao na Chad.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, (BMT),Dioniz Malinzi akisalimiana na katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki,Nicholas Musonye kwenye hafla hiyo fupi iliofanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano wa hotel ya New Africa,jijini dar.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti breweries Ltd,Teddy Mapunda akimkaribisha mgeni rasmi wa hafla hiyo,Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dionis Malinzi kwenye hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila kheri wachezaji wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi yao na Chad,sambamba na hafla hiyo SBL walizindua kampeni ya tangazo la televisheni iitwayo TUPO PAMOJA NA TUTASHINDA,hafla hiyo imefanyika kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa New Africa Hotel,jijini dar.


"Kiungo Mahiri " kampuni ya Serengeti,ambaye pia ni Meneja kinywaji cha Guinness,Moriss Njowoka akijaribu kuweka mambo sawa kabla ya mgeni rasmi na wageni mbalimbali kuwasili kwenye hafla hiyo jioni ya leo.
Wadau wa Timu ya Taifa nao walikuwepo kuitakia kila lakheri

Kocha wa timu ya Taifa,Jan Paulsen akisamiliana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Breweries,ambao ndio wadhamini wakuu wa timu hiyo, kwenye hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia kila kheri wachezaji wa Taifa stars kwa ajili ya mechi dhidi yao na Chad itakayochezwa N'djamena,Novemba 11 na baadaye marudiano yatakayofanyika Novemba 15 jijini Dar.


No comments: