Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL) Bw. Richard Wells (katikati) akitangaza hatua ya kampuni hiyo kudhamini mashindano ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge mwaka huu ambapo amesisitiza kwamba hii ni moja wapo ya malengo yaliyowekwa na kampuni hiyo yakiwa na nia ya kukuza na kuendeleza mchezo huo hapa nchini. Udhamini huo ni wa kiasi cha fedha za Kitanzania Shilingi Milioni 823. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano SBL Bi. Teddy Mapunda na Kulia Mwenyekit wa Bodi ya Wakurugenzi SBL Jaji Mark Bomani.
Katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya mpira wa Miguu Afrika Mashariki (CECAFA) Bw. Nicholas Musonye (wa pili kulia) akitoa shukrani kwa kampuni ya SBL kwa kudhamini mashindano ya kombe la CECAFA mwaka huu kupitia kinywaji chake cha TUSKER na kuipongeza kampuni hiyo kwa kuonyesha nia ya kukuza na kuinua vipaji vilivyopo Mashariki na Magharibi mwa Afrika. Kulia ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah, Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SBL Jaji Mark Bomani akifuatiwa na Rais wa TFF Leodgar Tenga.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki (CECAFA) Nicolas Musonye (kulia), akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 823 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Bw. Richard Wells katika hafla ya makabidhiano iliofanyika leo jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi (SBL) Jaji Mark Bomani na Kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano SBL Bi. Teddy Mapunda.
No comments:
Post a Comment