Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries,Teddy Mapunda akizungumza na baadhi ya wanahabari nje ya ofisi za TFF,Ilala jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kuihamasisha jamii kwa Taifa Stars iliyojulikana kwa jina la "Tuko pamoja na tutashinda"dhidi ya mchezo wao na timu ya Chad,utakaofanyika Novemba 1i jijini N'Djamena na baadaye Novemba 15 hapa jijini Dar,hiyo ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na mechi ya Kombe la Dunia.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Bw. Dioniz Malinzi akizindua rasmi kampeni ya kushangilia timu ya taifa Taifa Stars inaojulikana kwa jina la "Tuko Pamoja na Tutashinda", kwa ajili ya kusaka ushindi wa Taifa Stars katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Chard, utakaochezwa Novemba 11 na baadae Novemba 15 kufanyika mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kulia ni Maulid Kitenge mjumbe wa (BMT)Kocha wa timu ya taifa Jan Paulsen na kulia ni Rais wa TFF Leodger Tenga na katikati ni Mkurugenzi wa Mawasilano SBL Teddy Mapunda, uzinduzi huo umefanyika leo Karume jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries,Teddy Mapunda akizungumza mapema leo mchana,Maeneo ya Karume,Ilala Jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kuwahamasisha Watanzania kuishangilia timu ya Taifa,Taifa Stars iliyojulikana kwa jina la "Tuko pamoja na tutashinda"dhidi ya mchezo wao na timu ya Chad,utakaofanyika Novemba 1i jijini N'Djamena na baadaye Novemba 15 hapa jijini Dar,hiyo ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na mechi ya Kombe la Dunia.Timu ya Taifa Stars inadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Brewerie Ltd,kupitia kinywaji chake cha Serengeti Premium Lager.
Kocha wa timu ya taifa Jan Paulsen akizungumza machache kuhusiana na maandalizi ya timu hiyo yanavyokwenda sambamba na mipango mingine ya kuwaomba Watanzania kuishangilia timu yao ishinde dhidi ya mchezo huo,ambapo timu ya Taifa Stars leo imeingia Kambini kwa maandalizi makubwa.
No comments:
Post a Comment