Social Icons

Thursday 8 December 2011

DAKIKA 90 ZIMEKWISHA UGANDA NA KILIMANJARO STARS ZIKIWA SARE YA 1-1, SASA NI DAKIKA ZA NYONGEZA

Dakika 90 za mchezo zimekwisha katika uwanja wa Taifa kati ya Uganda The Cranes na Kilimanjaro Stars, Matokeo yakiwa sare ya kufungana goli 1-1, kwa matokeo hayo dakika 30 zimeongezwa na mpira unaendelea hebu tuone nani ataibuka mshindi na kuingia fainali akikutana na Rwanda ambayo tayari imeshakata tiketi ya kucheza fainali ya michuano hiyo ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 Jijini Dar es salaam baada ya kuifunga Sudan magoli 2-1.


Kama unavyoona makocha timu ya Uganda wakiwapasha misulia wachezaji wao kabla ya kuanza kipindi cha dakika 30 za nyongeza.
makocha timu ya Kilimanjaro Stars wakiwapasha misulia wachezaji wao kabla ya kuanza kipindi cha dakika 30 za nyongeza.
Mrisho Ngasa na wezake wakishangilia mara baada ya mchezaji huyo kufunga goli la kwanza.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA FULL SHANGWE BLOG

No comments: