Social Icons

Wednesday, 7 December 2011

Kifo cha Mr. Ebbo chazua bifu



Na Mwandishi Wetu
PAMOJA na kifo cha msanii, Mr. Ebbo, kuwasikitisha maelfu ya wapenda muziki nchini, hali ya kutoelewana ‘bifu’ kati ya wasanii wa Arusha na Dar es Salaam, imetanda kama vita baridi.

Mr. Ebbo, ambaye jina lake halisi ni Abel Motika Loshlaa, alifariki dunia wiki iliyopita katika hospitali ya Mount Meru, Arusha, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Baadhi ya wasanii wa miondoko ya hip hop, wamezungumza na gazeti hili na kuonyesha kukerwa na namna wenzao wa Dar es Salaam walivyoshindwa kujitokeza kwenye mazishi yake yaliyofanyika juzi huko Moshono mjini Arusha.

“Sidhani kama kunitaja jina ndiyo ishu, pointi yangu ya msingi ni hivi, Dar es Salaam wameonyesha ni wabaguzi na watu wasiojali,” alisema msanii ambaye anatokea Arusha lakini mara nyingi amekuwa jijini Dar.

Msanii mwingine maarufu anayetokea Arusha naye alisema hivi: “Kaka huwezi kuamini, wasanii kutoka Dar es Salaam utafikiri wamefanya mgomo. Kama huja Arusha kwa ajili ya shoo, vipi wanashindwa kuja kumzika mwenzao? Tena mtu kama Mr. Ebbo, ambaye hakuwa na makundi wala makuu, imetuuma sana.”

No comments: