Social Icons

Friday 2 December 2011

MSANII WA KUNDI LA ZE ORIJINO KOMEDY VENGU AZUSHIWA KIFO


Na Francis Godwin
Taarifa zilizozagaa mitaani katika mji wa Iringa na maeneo mengine hapa nchini zinadai kuwa msanii huyo Vengu ambaye hali yake ilikuwa mbaya amefariki dunia.

Taarifa hizi zimeonyesha kuwaliza wengi huku wadau mbali mbali wa mtandao huu wakipiga simu kutaka kujua usahihi wa taarifa hizo ambazo hata hivyo chanzo chake cha kuvumishwa bado kufahamika.

Hata hivyo jitihada za mtandao huu kumtafuta mmoja kati ya wasanii wa kundi hilo Emanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji bado zinaendelea ili kujua ukweli wa hali ya afya ya msanii huyo japo chanzo cha uhakika na cha karibu zaidi na familia ya Vengu kimedai kuwa hali ya afya ya Vengu kwa leo ni nzuri zaidi ukilinganisha na siku za nyuma.

Mtandao huu unaendelea kumwombea afya njema Vengu ili apone na kurejea kulitumikia Taifa katika tasnia ya sanaa

No comments: