Social Icons

Monday, 19 December 2011

Ukerewe mabingwa wa makasia ya Balimi Extra Lager

Mashaka Baltazar,Mwanza

Timu za wanaume, wanawake za Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza, zimetwaa ubingwa wa mbio za kupiga Makasia zilizofanyika Jijini hapa Jana na kuwapiku wapinzani wao, Kagera na Mara.
Kutokana na ushindi wa mbio hizo ambazo zimedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Balimi Extra Lager, Ukerewe ilijinyakulia zawadi za shilingi milioni 4.8
Akikabidhi zawadi kwa washindi Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, aliitaka TBL kuboeresha mitumbwi inayotumika katika michuano hiyo kuwa katika ubora unaofanana ili kuondoa malalamiko kwa washindani .
Alisema kuwa mitumbwi ikiwa katika ubora unaofanana itaondoa vishawishi kwa washindani kutumia dawa madawa ya kuongeza nguvu katika kupata ushindi.

Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuyaasa makampuni mengine kuona changamoto ya TBL ya kuinua michezo kwa kuiboresha ili ipindwe na wananchi, kwa vile michezo ipo ya aina nyingi na si mitumbwi pekee.

Ndikilo aliipongeza TBL kwa kutumia faida inayoipata kwa kushirikiana na jamii kupitia sekta ya michezo mbalimbali ili kutoa burudani, ukizingatia kuwa michezo mbali na burudani ni ajira lakini pia inatumika katika kujenga afya.
“Kampuni yoyote lengo kubwa ni kupata faida,pamoja na kupata faida hiyo ninyi mmeona vem,a kushirikiana na jamii kutokana na faida mnayopata.Nimeambiwa mnadhamini michezo ya ngoma za asili , baiskeli na juzi mmepandisha bendera ya taifa mlima Kilimanjaro katika kusherehekea mika 50 Uhuru, hivyo mnastahili pongezi” alisema Ndikilo
Kwa upande wa wanaume Ukerewe ilishika nafasi ya kwanza kutumia muda wa dakika 21:10 na kuzawadiwa kitita cha shilingi milioni 2.6, wanawake wao washika nafasi kama hiyo wakitumia dakika 25:38 na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 2.2

Kagera wanaume walishika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa dakika 21:15 hivyo kujipatia shilingi milioni 2.2 wakati Mara wanawake walishika nafasi ya pili wakitumia dakika 25:45 ambapo walipata shilingi milioni 1.6
Washindi wa watatu wanaume walikuwa Kisorya kutoka Mara ambao walitumia dakika 21:38 na kupata shilingi milioni 1.6,wakati wilaya ya Ukerewe timu ya pili wanawake ilishika nafasi ya tatu na kutwaa kitita cha shilingi 800,000 wakitumia dajkika 26:24.
Aidha washindi wengine wa nafasi ya nne wanaume kutoka musoma walipata zawadi ya shilingi 850,000 wanawake kutoka Ilemela Mwanza wakiambulia shilingi 600,000, ambapo waliotinga fainali kuanzia nafasi ya tano hadi kumi walipata lifuta jasho cha shiingi 200,0000.
Mkoa wa Mwanza umekuwa mwenyeji wa mbio hizo za mitumbwi tangu ilipoanzishwa na TBL , ambapo fainali ya michuano ya mwaka huu ilishirikisha timu 26 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara na mkoa wa kimichezo wa Ukerewe ambao wametwaa ubingwa huo.

No comments: