Timu ya Yanga |
Mishahara hiyo ambayo wachezaji wanadai ni ya mwezi Novemba na Desemba, ambao umeambatana na sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata ni kwamba mbali na wachezaji hao, pia wafanyakazi wengine walioajiriwa na klabu hiyo hawajalipwa kwa muda wa miezi mitatu sasa.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa hali hiyo ya ukata imechangia mambo mengi kutofanyika kama ilivyotarajiwa ikiwemo kuvurugika kwa programu ya mazoezi.
"Hali ni mbaya, klabu haina pesa, mambo mengi hayafanyiki kama ilivyokusudiwa, tunajaribu kufanya kila linalowezekana ili kutatua tatizo hili linalotukabili," alisema mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Aliongeza kuwa kukosekana kwa fedha kutoka kwa aliyekuwa mfadhili wao na mapato madogo ya mlangoni yaliyokuwa yakipatikana katika mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi ndio sababu nyingine iliyofanya klabu yao ikose fedha za kujiendesha.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment