
Bango linavyoonesha matokea hadi dakika ya mwisho.kufuatia matokea hayo yainaiperekea timu ya Zanzibar Heroes kuachia ngazi mashindano hayo,huku yakiwa yamebaki matumaini kwa timu moja ya Tanzania Bara iliyobaki,ambapo hapo kesho inashuka dimbani kuchuana na timu ya Malawi.Wakati huo huo timu ya Sudani imefuzu katika hatua hiyo ya robo fainali kwa kuichapa timu ya Burundi goli 2-1,katika michuano ya CECAFA Tusker Challenge Cup 2011 inayoendelea kufanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mchezaji Abdul Halim Humoud kutoka timu ya Zanzibar Heroes akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Rwanda,Gasana Eric wakati timu hizo zilipokuwa zikichuana vikali jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar,katika kuwania hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya CECAFA Tusker Challenge Cup 2011.
No comments:
Post a Comment