Social Icons

Tuesday 17 January 2012

Airtel yazindua rasmi huduma ya kununua mafuta ya gari kwa Airtel Money katika vituo vya Gapco











Mteja
wa Airtel money Bw David Ramadhani akitumia simu yake ya Airtel
kununua mafuta ya gari kwa kutumia huduma ya Airtel money katika kituo
cha Gapco jijini Dar-es-salaam. Anaemuwekea mafuta ni muhudumu wa kituo
hicho Bi. Nina Owiso na wa kwanza kushoto ni Mercy Nyange Afisa
Uendeshaji wa Airtel Money akishuhudia mara baada ya hafla ya uzinduzi
wa huduma hiyo ya kununua mafuta kwa kutumia Airtel Money katika vituo
vya Gapco Dar es salaam iliyofanyika mwishoni mwa wiki.







Meneja
uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Bw Jackson Mmbando akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu huduma ya kununua mafuta ya gari na ya
taa kupitia huduma salama,rahisi na ya haraka ya Airtel money jijini
Dar-es-salaam jinsi wanavyoweza kufaidika na huduma hiyo ambayo
itawarahisishia maisha ya kila siku kuepuka kutembea na pesa nyingi
mifukoni lakini wakiwa na huduma hiyo wanaweza kuepuka usumbufu huo .
uzinduzi rasmi wa kununua mafuta kwa kutumia Airtel Money katika vituo
vya Gapco Dar es salaam umefanyika mwishoni mwa wiki




======= ====== ==========


Akiongeawakati wa kuvitangaza vituo vitakavyotoa huduma hio kwa sasa jijini Dares alaam kwa waandishi wa Habari Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson

Mmbando alisema " Lengo letu Airtel kupitia Airtel Money ni kuhakikisha
huduma hii ya Airtel Money inakuwa suluhisho la kudumu kwa




mahitaji ya kila siku kwa wananchi wote na wateja wetu kwa ujumla.


Sasaunaweza kupata huduma katika vituo vya Gapco Dar es salaam pale Sasakazi-Mtoni Mtongani, Gapco Banana-Gongo la Mboto, na Gapco-bara bara ya
Samora Lengo letu baada ya miezi miwili ijayo tuwe tumesambaza huduma
hii ya


kununua mafuta kwa Airtel Money katika kwa vituo vingi zaidi na watoa huduma hii wote! Aliongeza kusema Mmbando.



Mbalina kutoa huduma ya kununua Mafuta kwa Airtel money vituo hivi pia niWakala wetu ambao pia mteja ataweza kutoa au kutuma fedha wakati wote
vituo hivi vinapokuwa wazi


MenejaMauzo wa GAPCO, Mr Ben Temu alisema "huduma ya kununa mafuta ni rahisikupitia Airtel Money, Wateja wote wa Airtel tunawakaribisha katika vituo
vyetu vya Sasakazi- mtoni mtongani, banana-Gongo la Mboto na kile cha
Bara bara ya samora mjinunulie mafuta kwa kupitia Airtel
Money
Aaliongezakwa kusema " Ninaipongeza sana Airtel kwa kuja na huduma hizi borazinazoonyesha ubunifu wa hali ya juu sasa hii inatupunguzia hatari yakutembea na kiasi kikubwa cha pesa kadhalika hata wamiliki au
wafanyabiashara wa petrol na disel kama sisi" alisema Mr Temu

No comments: