
Huu ni Mkia wa Mbuzi ambao umenona sana na kwa bei yake ya kilo moja ni Tsh: 15,000 na watu wanavamia sana

Kichwa cha Moo kikiwa Dukani Ambapo pia watu wanakuwa wengi sana kutaka kununua

Hii ni Baadhi ya minofu iliyo katwa katwa ambapo mteja anachagua vipande anavyo taka anapimiwa kwa kilo kisha anaondoka zake

Hii ni mashine maalum inayo tumika kukatia Nyama hizo, na mifupa migumu migumu

Hawa ni kuku ambao wanangojea kununuliwa katika eneo hilo la soko la jioni wanaonekana ni wengi lakini baada ya masaa kadhaa wote hutoweka kwa kununuliwa

Huu ndio Muonekano wa Maduka hayo mbali Mbali ambapo wanauza kila kitu ikiwemo kuku na mengineyo mengi

Hapa sasa ni muonekano baadhi ya vitu kutoka kwa kuku kama vinavyo onekana kuna Firigisi, Maini na Miguu ya Kuku hakuna kinacho tupwa hata nyongo ina kazi ingine kwa hiyo nayo inahifadhiwa

Hizi ni Kongoro za Moo ambazo zipo tayari kabisa kwa ajili ya kuuzwa, zilikuwa zimejaa eneo hilo lakini wadau wamezishambulia
No comments:
Post a Comment