Social Icons

Sunday, 15 January 2012

Klabu ya Rose Garden ya mjini Dodoma waibuka mabingwa wapya wa mashindano ya Darts taifa kwa mwaka 2012

Mabingwa wapya wa Mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale (Darts) kwa mwaka 2012,wakiwa kwenye meza picha ya pamoja na baadhi ya vingozi wa Taifa wa Mchezo huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa,Gesase Waigama (wa pili kushoto waliokaa) mara baada ya kukabidhiwa kombe lao wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa Rose Garden,mjini Dodoma.Wengine ni Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa na ubao wa Darts ikiwa ni sehemu ya kushangilia ubingwa wao huo.
Nahodha wa timu ya Rose Garden ya Mkoani Dodoma ambao ndio Mabingwa wapya wa Mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale (Darts) kwa mwaka 2012,Carlos Paranjo akipokea Kombe la ubingwa huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa,Gesase Waigama wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Rose Garden,mjini Dodoma.Wengine ni Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa na ubao wa Darts ikiwa ni sehemu ya kushangilia ubingwa wao huo.
Wachezaji wa Timu ya Safari kutoka Mkoani wa Mwanza ambao ni Washindi wa Pili wa Mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale (Darts) wakishangilia ubingwa wao huo mara baada ya kukabidhiwa kikombe na Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa,Gesase Waigama wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Rose Garden,mjini Dodoma.
Bingwa wa Mchezaji wa Mmoja Mmoja wa Mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale (Darts) kwa upande wa wanawake,Fabiola Namajojo kutoka Mzinga Mkoani Morogoro,akikabidhiwa kikombe chake cha ushindi huo na Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa,Gesase Waigama wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Rose Garden,mjini Dodoma.
Bingwa wa Mchezaji wa Mmoja Mmoja wa Mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale (Darts) kwa upande wa Wanaume,Aderade Chikoma kutoka mkoani Mbeya,akikabidhiwa kikombe chake cha ushindi huo na Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa,Gesase Waigama wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Rose Garden,mjini Dodoma.

No comments: