Social Icons

Thursday 12 January 2012

Mkuu wa Boko Haram atetea mashambulio

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislam wenye itikadi kali nchini Nigeria, Boko Haram, ametetea mashambulio dhidi ya Wakristo ya hivi karibuni, akisema ni ulipizaji kisasi wa kuuawa kwa Waislam.
Katika ujumbe wake wa kwanza kupitia video, ambao umetolewa kwenye wavuti wa YouTube, kiongozi huyo Abubakar Shekau ametaja mashambulio dhidi ya Waislam katika miaka ya hivi karibuni katika maeneo kadhaa kaskazini mwa Nigeria
Wanamgambo wa Boko Haram walishambulia makanisa kadhaa siku ya Krismasi, na kuua waumini wengi.
Hali ilisababisha kutokea kwa mashambulio ya kulipiza kisasi katika isikiti, hasa katika maeneo ya kusini yenye Wakristo wengi.
Kwa hisani ya BBC SWAHILI


No comments: