Social Icons

Friday, 27 January 2012

Twiga star Yaitandika Bunge SC 2-1 mchezo wa hisani,yachangiwa sh mil 7

Nahodha wa timu ya Twiga Stars, Sophia Mwasikili akionesha kitita cha shilingi milioni 7 alizokabidhiwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu,kwa niaba ya timu ya Wabunge..
Kikosi cha timu ya Bunge SC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, ambao ulikuwa ni maalumu kuichangia timu hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Twiga Stars imeshinda 2-1.
Kikosi cha Twiga Stars kikiwa katika picha ya pamoja.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, akipeana mkono na mshambuliaji wa Twiga Stars, Mwanahamis Omari.
Wachezaji wa Bunge SC, Halima Mdee na William Ngeleja, wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mchezo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza kabla ya kukabidhi kitita cha sh. milioni 7 kwa wachezaji wa Twiga Stars.
Nahodha wa timu ya Twiga Stars, Sophia Mwasikili, akionesha kitita cha sh. milioni 7 baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri, Ummy Mwalimu (kulia).
Mlinzi wa timu ta Twiga Stars, Siajabu Hassan akimtoka mshambuliaji wa Bunge SC, Adam Malima.
Mshambuliaji wa Bunge SC, Sadifa Juma Khamis akimtoka beki wa Twiga, Fatuma Khatib.
Mshambuliaji wa timu ya Bunge SC, Adam Malima akimtoka beki wa timu ya Twiga Stars, Siajabu Hassan wakati wa mchezo wa hisani ambao ulikuwa ni ni maalumu kwa kuichangia timu ya Twiga Stars uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Twiga Stars imeshinda 2-1.
Picha zote kwa hisani kubwa ya James Dande wa Globu ya Jamii.

No comments: