Social Icons

Tuesday, 21 February 2012

Mambo Yalivyokuwa Dar Live Jumapili





MOTO mkali uliendelea kuwaka kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala jijini Dar usiku wa Jumapili ambapo wasanii mbalimbali wa Bongo: Linex, Khadija Kopa, Alex Machejo, na makundi ya ngoma za asili ya Machozi na Mawazo Group, bendi ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’, Dogo Lila na msanii Kidum kutoka nchini Burundi, wote hao walikamua sambamba na washiriki wa shindano la ‘Vaa, Imba na Cheza,Kama Rihanna’ na kuufanya umati mkubwa ulifoka hapo kupata burudani isiyopimika katika hali yoyote.

Wasanii hao walitumbuiza kwenye Family Day Bonanza ambalo hufanyika kila siku ya Jumapili chini ya usimamizi wa uongozi wa kituo hicho cha Dar Live kilichopo Mbagala-Zakheem jijini Dar es Salaam


Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

No comments: