Social Icons

Monday 13 February 2012

TUNDAMAN APAGAWISHA MASHABIKI 'UWANJA WA NYUMBANI' JIJINI LONDON


Mambo yalikuwa moto moto
Mashabiki wakijiachia
Msanii wa Bongo Movie Meckyladiva akionyesha support yake.
Tundaman akiwapagawisha mashabiki waliohudhuria show yake.
Warembo Naju, Rahma, Shenaz na Jestina George wakiwa kwenye show.

Msanii Tundaman yuko nchini Uingereza kwaajili ya show iitwayo 'Tundaman Valentine Tour' iliyo andaliwa na mwanadada Safina Kassu wa Kassu Entertainment. Show yake ya kwanza ilianza jana tarehe 11 Feb 2012 katika kiota kipya cha maraha jijini London kiitwacho The Pit Stop 'Uwanja Wa Nyumbani' ambao msanii huyo alikoga nyoyo za masahbiki wake pale alipo anza makamuzi na kuwashukia na nyimbo zake pamoja na za kikundi cha Tip Top Connection.

Show zinaendela na tunaomba watu wajitokezee kwa wingi kwa ajili ya kumsupport msanii na mtanzania mwenzetu huyu.
Picha na Jestina George Blog

No comments: