Social Icons

Sunday 29 April 2012

CHEKA ‘AMPOLA’ GARI MAUGO APATA NALO AJALI USIKU HUO HUO WA JANA


 Gari la Cheka likiwa Kituoa cha Polisi Magomeni baada ya kupata ajali jana usiku.
***************************
*Furaha ya ushindi wa Cheka kumchapa maugo yaishia kituo cha Polisi
*Alala Oysterbay Polisi adhaminiwa leo
 BAADA ya Bondia mahiri  Francis Cheka kuibuka na ushindi mnono wa TKO dhidi ya mpinzani wake Mada maugo na kukabidhiwa mkanda wa ubingwa wa Afrika Mashariki IBF na Gari lenye thamani ya Sh. Milioni 8, katika pambano lao lililofanyika jana usiku katika Ukumbi wa PTA, furaha ya bondia huyo iliishia mikononi mwa Polisi.

Ikiwa ni siku moja tu baada ya kuvishwa taji la ubingwa huo na kukabidhiwa mchuma wake, Cheka alikamatwa na Polisi masaa machache tu baada ya kukabidhiwa gari na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake ambayo iliishia mitaa ya Manzese baada ya kupata ajali kwa kugonga Pikipiki na kuwajeruhi dereva wa pikipiki hiyo na abiria wake ambao walikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.


ZAIDI SOMA HAPA CHINI
Sufian Mafoto

No comments: