Social Icons

Monday 30 April 2012

KUJITOA KWA MWANA-FA TFU KWA MUEPUSHIA BALAA LA ANTI-VIRUS VOL 3


Mwanamuziki wa Hip hop mwenye mafanikio ya aina yake katika industry ya muziki wa kibongo, Hamis Mwinjuma a.k.a MwanaFA ameondolewa kwenye list ya watu ambao walipaswa kuchanwa kwenye volume three ya Anti-Virus ya Vinega.

MwanaFA ambaye alikuwa centre ya michano katika volume iliyopita iliyopata mafanikio makubwa, safari hii ameondolewa kwenye hiyo list baada ya kujitoa rasmi TFU ambayo ni kampuni ya wasanii yenye dhamana ya kusimamia inayosemekana studio iliyotolewa na mwenye nchi yake. TFUama Tanzania Fleva Unit na ilipata wakati mgumu sana pale Mh Sugu alipoilipuwa bungeni huku umati wa Tanzania ukikodoa macho kwenye kideo.

Akizungumza na KaribuNdani Kinega kiongozi Peenlawyer amesema Mwana FA sio target tena kwani kashajitoa TFU ila moto utawaka kwa Kusaga, Nchimbi na utawaka zaidi kwa Ruge, mameneja masoko, Kili Awards na baadhi ya watangazaji ambao wamekuwa chachu ya rushwa na unyanyasaji wa wasanii..

Volume 3 iko njiani na kinachofanywa kwa sasa ni kujipanga ili kuangalia muda muafaka wa kudondosha hiyo mix-tape.
Habari kwa Hisani ya Chuma Blog

No comments: