Ndugu zangu,
Nimehuzunishwa na picha za Mahakamani kwenye magazeti ya jana zikimwonyesha msichana Elizabeth ' Lulu' Michael akilia hadharani.
Nikivaa miwani ya mzazi nilimwona mtoto ambaye angeweza kuwa wangu. Nilimwona mtoto anayedhalilishwa mbele ya macho ya jamii. Nilimwona mtoto anayehukumiwa na jamii ambayo hadi sasa haijui ukweli wa kilichotokea.
Jamii inapaswa kujiuliza, kwa nini picha za Lulu akiwa analia zina umuhimu kwa wanajamii kuziona?Je, ni kwa sababu machozi ya Lulu ni dhahabu kwa wengine? Kwamba yanasaidia kwenye kuuza magazeti? Je, kuwa na huzuni na kutoa machozi si haki ya hisia za mwanadamu ambazo zinapaswa kuheshimiwa? Kwa nini ziwekwe hadharani? Hicho ndicho jamii inataka kukiona? Na ikishaona?
Tutafakari.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
No comments:
Post a Comment