Wanajeshi zaidi ya1000 wa Sudan Kusini wamekufa katika mapigano dhidi ya Majeshi ya Sudan katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Heglig.
Wanajeshi wa SPLM waliouwa wamefikia1200 mwishoni mwa juma wakati Sudan Kusin ikidai kuwa inajiondoa katika eneo hilo. Huku ikiwa kimya kuzungumzia juu wanajeshi wake waliouwawa katika mapigano hayo ya mataifa ndugu.
Katika siku ya kumi ya umiliki wa Heglig Sudan Kusin ilidai kuwa wanajeshi wake waliofariki ni kumi tu na wanajeshi 240 wa Sudan waliwaua. Kwa hakika imekuwa vigumu kujua waliouwawa lakini kulinga na taarifa za mwanahabari kutoka shirika la Habari la Ufaransa (AFP) anasema eneo hilo lilikuwa na mili mingi ya maiti za wanajeshi wa Sudan Kusini. Huku akiwa na picha wanajeshi zaidi 100 toka Sudan wakipata matibabu mjini Khartoum.
Kulingana na taarifa za mmojawapo wa wasaidizi wa Rais Omar Al Bashir kwa Shirika la Habari la Sudan anasema idadi ya wanajeshi wa Sudan Kusini pamoja na mamluki wake waliouwawa kwa sasa wanafikia 400.
Hapo awali Sudan ikikataza kabisa vyombo vya habari katika eneo hili na jumamosi taifa hilo likasema kuwa limemaliza kazi ya kuwafurusha wanajeshi wa Sudan Kusini katika eneo lao la Heglig ambapo Sudan Kusini ilidai kuwa ni eneo lake katika mkoa wa Abyei.
Sudan Kusini iliteka eneo hilo April 10 mwaka huu kufuatiwa na madai yake ya ndege za Sudan kushambulia taifa hilo na baadae jumuiya ya kimataifa iliingilia kati mgogoro huo.
Chanzo DW Swahili
No comments:
Post a Comment