Diamond na mama yake waki beba vitu kupeleka kituoni hapo
Diamond akiwa amepakata mtoto mmoja wapo wa kituo hicho
Diamond na Meneja wake Joff wakiwa wamepakata watoto wa kituo hicho
Diamond na meneja wake wakikabidhii misaada
Meneja wa Diamond Joff akikabidhii msaada huku Diamond, mama yake mzazi, pamoja na mmoja wa wasimamizi wa kituo hicho wakiangalia
Baadhi ya watoto wakiwa katika picha na misaada aliyoitoa Diamond
Mtoto wa kituo hicho akisoma dua baada ya kupokea misaada
Diamond akiwa ana cheza na mtoto mmoja wapo kituoni hapo
Mtangazaji wa Clouds Tv, Shedee akibadilishana mawazo na mtangazaji mwenzake
Diamond akisign kitabu cha wageni
---
Star wa Bongofleva Naseeb Abdul ‘Diamond’ jana alitoa
msaada katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre
kilichopo Kinondoni Hananasif jijini Dar.
Akizungumza na mtandao wa globalpublishers kabla hajakabidhi msaada huo, Diamond alisema kuwa kikubwa zaidi kilichomfanya hadi atoe msaada ni kuguswa na maisha wanayoishi yatima hao.
“Unajua siku zote Mungu anasema unachokipata ugawane na wenzako, sasa mimi pamoja na meneja wangu Joffrey a.k.a Joff tumeona tutoe nusu ya kile tulichokipata kwa hawa ndugu zetu wanaolelewa katika kituo hiki,” alisema Diamond.
PICHA /HABARI: SHAKOOR JONGO WA GPL.
No comments:
Post a Comment