Social Icons

Wednesday, 30 May 2012

DIAMOND KUTUMBUIZA KATIKA SHINDANO LA MISS CHANG'OMBE


Baada
ya  kufanya  show ya Big Brother  Afrika Kusini MSANII Abdul Naasib
‘Diamond’ni mmoja wa wasanii watakaotoa burudani kamambe kulipamba 
shindano la Redd’s Miss Chang’ombe 2012 shindano litakalofanyika Juni 9
mwaka huu  katika ukumbi wa Quality Centre barabara ya Nyerere Jijini
Dar es Slaam.

Wengine
watakaopamba shindano hilo la aina yake ni  kundi la Original Commedy
akina Joti na bendi ya mapacha watatu ambayo kwa sasa imekuwa moja ya
bendi zinayokonga  nyoyo za mashabiki wengi wa muziki hapa nchini.

Akizungumza
Jijini Dar es Salaam msemaji wa Kampuni ya King Promoters  ambao ndiyo
waandaaji wa shindano hilo Martin Mauya ameaema kuwa kwa sasa warembo
hao wameendelea kufanya mazoezi katika viwanja vya klabu ya TCC
Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.

Shindano
hilo linatarajia kushirikisha warembo bomba 14 watakaopanda jukwaani
kuchuana vikali kumpata mrembo wa mkoa huo wa kimashindano wa Chang’ombe
huku baadhi ya wadau wa fani hiyo ya urembo nchini wakitabiri kuwa
mrembo wa Tanzania mara hii atatokea katika mkoa huo wa kimashindano.

Mauya 
amewataja warembo wanaotarajia kupanda jukwaani ni Elizabeth Mushi,
Restituta Faustine, Miriam Ntakisivya, Flora Kazungu, Flora Robert, 
Like Abraham, Clara Diu, Margareth Gerald, Jesca Haule, Deborah
Nyakisinda, Suzan Paul, Wensley Matius, Zulfa Bundara na Catherine
Masumbigana.

‘Kwa
sasa warembo hao wanafanya mazoezi na kurudi nyumbani lakini Juni 3
warembo hao wataingia rasmi kambini katika Hoteli moja kubwa Jijini
kabla ya kuapnda hiyo Juni 9’ alisema Mauya.

Shindano hilo limedhaminiwa na REDD’S
ORIGINAL, NEXUS CONSULTING AGENCY, DODOMA WINE, CXC AFRIKA, PAPAZII
INTERTAINMENT, KITWE GENERAL TRADERS,CHERISH, BEN EXPEDITION, SCREEN
MASTERS, ARDHI PLAN LIMITED.

No comments: