Social Icons

Sunday, 13 May 2012

Happy Mother's Day:Mimi pia Nasherekea Siku ya Mama Duniani. Je umemfanyia nini Mama yako?

Nikiwa na Umri wa Miezi Nane

Siku zote hakuna mwanadamu Aliye Zaliwa akiwa na miaka 20 ama hamsini Mbele kila mmoja wetu alizaliwa na kuanza na mwaka Zero
Tukiwa watoto tumepata malezi Bora kutoka kwa mama zetu wametutunza Vema mpaka na sisi tukaitwa watu wazima .
Binafsi na penda sana Kumshukuru mama yangu kwa malezi Bora mpaka nimefikia hapa sasa na mimi kuitwa mtu mzima, Lakini pia napenda kumshukuru sana Marehemu Baba Yangu ambaye pia amenitunza Vema na yeye pamoja na Mama kunisisitiza juu ya Elimu, Upendo na kuishi vema na watu.
Hivyo basi ni Vema kila mmoja wetu kujua na Kumshukuru mama mzazi ambaye ndiye aliye tubeba kwa Umri wa miezi Tisa mpaka tunakuja duniani na kuendelea kuishi.
Umri Umekwenda na sasa na mimi naitwa mtu mzima

Katika siku hii Muhimu kabisa ya Mama Duniani napenda kuwapa Pole wakina mama wote ambao wananyanyaswa na watoto wao walio wazaa wao wenyewe, Ambao kwa Bahati mbaya hawakubahatika kuwa na watoto kwa watoto  wao Kupoteza maisha kwa Njia mbali mbali, Pamoja na wakina mama wote Wajane ambao hawana waume zao.

Mwisho Kutoka kwa Blog yangu inaungana na watu wote popote duniani katika Kusherekea Siku ya Mama Duniani .
Imetolewa na 
Fredy Tony Njeje



No comments: