Social Icons

Tuesday, 29 May 2012

KIJANA MDOGO MKAZI WA KIGOGO AJINYONGA NA KUFARIKI KISA NI UGUMU WA MAISHA


Marehemu akionekana kwa nyuma.
Mke wa marehemu akilia kwa uchungu.…
MWANAMME mmoja ambaye hakutambulika jina lake, aliyekuwa mkazi wa Kigogo-Mbuyuni jijini Dar es Salaam asubuhi ya kuamkia leo (Mei 29), amejinyonga kwa madai ya ugumu wa maisha uliosababishwa na kukosa ajira.
Wakizungumza na mtandao wa huu, baadhi ya majirani ambao walihojiwa walisema kuwa jamaa huyo kwa muda mrefu alikuwa hana kazi hivyo kumsababishia ugumu wa maisha ambao ulikuja kumfanya ajinyonge.
“Siku zote mwanaume ameumbwa kutafuta riziki na si kukaa kusubiri kuletewa riziki. Jamaa huyu alikuwa akikaa tu nyumbani akimuachia mkewe aende akatafute riziki, matokeo yake ndio haya,” alisema jirani mmoja aliyekuwepo eneo la tukio.
(Picha/ Habari: Shakoor Jongo /GPL)

No comments: