Social Icons

Saturday 19 May 2012

MADOGO WAJIFUA VEMA TAYARI KWA MASUMBWI KINONDONI






 Katika picha juu na chini ni baadhia ya mabondia chipukizi wa bigright boxing na
mwalimu wao IBRAHIM KAMWE wakimalizia mazoezi yao ya mwishomwisho kwa

ajili ya mpambano wa ngumi unaotegemewa kufanyika jumapili20/05/2012
katika ukumbi wa Vijana Hall kinondoni wakisindikiza pambano la
ubingwa wa taifa wa Bantam weight chini ya usimamizi wa TPBO kati ya
RAMADHAN KUMBELE na JAMES MOKIWA raundi kumi.vijana hao wameahidi
kuonesha mchezo mzuri wa ushindi 'kama ilivyo kawaida yetu ushindi
kwetu ibada'
Mabondia hao wanaotegemea kupima uzito jumamosi19 katika ukumbi wa
STEREO club-kinondoni na Heavy weight Anord'biggie'120kg v/s Karim'big
paquiao118kgs raundi sita, feather weight-Doi miyeyusho v/s Jumanne
Mtengela, Light weight Jafar Majia v/s Daudi Muhunzi, Fly weight-Sadat
miyeyusho v/s swed hassan,Martin Richard v/s Yohana Thobias na
mapambano mengi mengineyo yakiwemo ya watoto na Burudani toka kwa
KARAPINA,MAKHIRIKHIRI WA KIBONGO NA TID.
mapambano haya yote yameratibiwa na Tasenga na BigRight Promotion kwa
lengo la mfululizo wa mapambano ya kuinua vipaji vya mabondia wa
Tanzaniana kutafuta mabingwa wa taifa kabla ya kimataifa.

No comments: