Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete, akiwapa somo la kucheza na kufunga magoli wakati alipowatembelea kwenye kambi yao ya mazoezi wakijiandaa kwa michuano ya Afrika itakayofanyika hapa nchini hivi karibuni.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia mazoezi ya timu ya taifa huko Kibaha walikopiga kambi yao.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya netiboli,Taifa Queens, wakati wakifanya mazoezi kwenye kambi yao iliyoko katika shule ya sekondari ya Philbert Bayi huko Kibaha wakati alipowatembelea
Mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete, akimkabidhi mchango wa shilingi milioni kumi, Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi, kwa ajili ya maandalizi ya timu ya taifa ya mchezo huo. Makabidhiano hayo yalifanyika huko Kibaha tarehe 4.5.2012 ambako timu hiyo imeweka kambi.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete, akifuatana na wake wa Makamu wa Rais,Zakhia (wa pili) na Asha Bilali (wa mwisho) wakiagana na wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli huko Kibaha.
Picha na John Lukuwi
No comments:
Post a Comment