Social Icons

Thursday, 31 May 2012

SAJUKI AFANYIWA UPASUAJI.

Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ hospitalini.
Na Erick Evarist
HATIMAYE, staa wa filamu za Bongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefanyiwa upasuaji wa tumbo kufuatia matatizo yanayomsumbua, Amani limeambiwa na Wastara.
Akizungumza Jumatatu iliyopita kwa njia ya simu tokea Mumbai, nchini India alikolazwa mumewe, mke wa Sajuki, Wastara Juma alisema madaktari wamefanikisha upasuaji huo, lakini hali ya mgonjwa huyo ikawa mbaya ghafla.
Aliongeza kuwa kufuatia hali hiyo, maombi yanahitaji kwa Watanzania ili mumewe arejee katika hali inayotazamiwa na madaktari.
Hata hivyo, Jumanne iliyopita, Wastara alizungumza tena na mwandishi wetu ambapo alisema Mungu ni mkubwa, hali ya mumewe anatengemaa na ameanza kunyanyuka baada ya upasuaji huo.
“Hali imekuwa nzuri, sasa ananyanyuka si kama alivyotoka kwenye chumba cha upasuaji, lakini Watanzania wazidi kumwombea,” alisema mwanadada huyo.
Katika hali nyingine isiyokuwa ya kawaida, Wastara alisema akiwa hospitalini hapo, madaktari wameidaka kamera yake na kuiweka mapokezi wakimtuhumu kuitumia vibaya.
Walimwambia kuwa ni kosa kwa mtu kutumia kamera yake kupiga picha bila ridhaa ya utawala. Hata hivyo, msanii huyo alisema atarudishiwa kifaa chake hicho cha kuchukulia picha kwani alitoa barua kutoka Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’ inayoonesha yeye ni msanii wa muvi nchini.
Sajuki, yuko nchini humo akitibiwa matatizo ya vimbe tumboni. Aliondoka nchini katikati ya Mei, 2012 kwa ajili ya kufuata matibabu.
Kwa hisani ya Global Publishers

No comments: