Timu ya Azam Fc leo imelambishwa maji ya miwa na Mtibwa Sugar katika mchezo uliokuwa wa marudiano baada ya ule uliovuvjika wiki iliyopita katika Uwanja wa Chamazi, ambapo Mtibwa Suga wameibuka Kidedea kwa kuwachabanga mabao 2-1 na kupoteza matumaini ya Azam Fc kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012. Babao wa Mtibwa Sugar yamefungwa na Waziri Ally na la pili likitupiwa na Juma Abdul, huku bao la Azam Fc likiwekwa kimiani na John Boko. Kwa matokeo hayo sasa Simba imejikatika tiketi ya kutwaa Ubingwa bila ya mpinzani, huku wakisubiri kumalizia mchezo wao wa mwisho katika msimu huu wa Ligi Kuu na Mahasimu wao wa Jadi Yanga, mchezo unaotarajia kupigwa siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam.
Habari kwa Hisani ya Sufiani Mafoto Blog
Habari kwa Hisani ya Sufiani Mafoto Blog
No comments:
Post a Comment