Social Icons

Saturday, 12 May 2012

Timu ya Tanzania DMV watachuwana vikali na timu ya Ethiopia Kundi (B)


Na Abou Shatry

Katika
mchezo wa lingi ya 2011 Diaspora World Cup zinazoendelea katika viwanja
vya Hyattsville na Germantown jijini Maryland Nchini Marekani, timu ya
Tanzania DMV watachuwana vikali na timu ya Ethiopia Leo hii Jumamosi May
12, 2012 mida ya 12:PM (Mchana wa saa sita) katika kiwanja cha
Greencastle, kiliopo Burtonsville, Maryland
  
Kundi
(B) Timu ya wa Ethiopia katika mchezo wa awali walifungwa bao 3-0 na
timu ya Malawi ndani ya uwanja cha  Greencastle, Burtonsville, Maryland,
ambao leo watajianda vikali ili kutaka kurudisha nguvu zao kwa mchezo
waliopoteza dhiti ya timu hiyo ya Malawi, ambao leo hii timu ya Malawi
watapambana vikali  na timu ya Armenia mida ya saa 1:PM Mchana wa leo,
kwa mechi ya kwanza timu ya Armenia waliwabamiza Nigeria bao 4-1 katika
mchezo wa awali.

Pia
timu ya waTanzania DMV katika mchezo wa kwanza siku ya Jumapili ya
April 29,2012 walifanikiwa kuwabamiza timu ya Ghana bao 3-2 ndani ya
uwanja wa SoccerPlex Stadium uliopo Ager Road Hyattsville Maryland.

Kama
kawaida  yao timu ya waTanzania DMV inawaomba Watanzania wote
ushirikiano wenu wa kila hali ili kuipa changamoto timu ya Watanzania
DMV, mnaombwa pia kufika mapema mida ya saa 11:AM  kuzowea mazingira
kabla ya mchezo huo kuanza.

Adress ya mchezo utakaochezwa leo hii ni Fairland Field 3928 Greencastle Rd. Burtonsville, Maryland  20866 Habari na http://swahilivilla.blogspot.com/

No comments: