
Hadija Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma Mkatoliki AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa kutwaa Tuzo mbalimbali za Kili Music 2012. Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio hilo.
Pichani juuni Mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.

Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.

Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Kilimanjaro.

DJ Choka akisugua vyombo kuendana na Roma Mkatoliki

Hapa ni usiku ....

...ni mchana

anastua...huyu ni Gwiji Hadija Kopa akifanya vitu vyake jukwaani hapo Ushirika. Mama alifunika mbaya katika show hii

Wakali wa ragge kutoka kundi la Warriors from East la mjini Arusha wakitumbuiza mashabiki katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.

Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza show wake wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.

Hawa nao walikuwa wakitoa mpya ya kujirusha na kuangukia mgongo. Ni vijana wa Suma Lee.

Suma Lee akifanya vitu vyake jukwaani


Msanii anae kuja juu Omy Dimpoz nae akikamua jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba leo.

Nai Nai hapa ikiimbwa maana Omy Dimpoz alimshirikisha Ali Kiba

Wadau wakifuatilia show hiyo

Ali Kiba akienda sawa na vijana wake, hakika Moshi ilikuwa hapatoshi.
Picha/Habari Kwa Hisani ya Father Kidevu Blogu
Picha/Habari Kwa Hisani ya Father Kidevu Blogu
No comments:
Post a Comment