Sehemu ya kwanza
Angalieni sana hii kitu inaitwa Facebook aisee,wote wadada na wakaka,kuna vitu vya ajabu sana vinaendelea humu...Kuna wadada wanajiuza wako humu ni wewe tu na muda wako unapewa huduma unalipia...Kuna wachawi humuhumu...Kuna freemasons humu wakikutumia Friend request uki-accept tu uko hatarini kufa...Kuna mengi sana sana!
Kwa leo kuna hili tukio linaloripotiwa kutokea Mwanza,siku chache tu nyuma...
Kuna Mwanafunzi wa kike,mrembo kweli wa chuo almaarufu pale Mwanza kinaitwa Mtakatifu Augustino....Amekutana na Mwanaume Facebook,wakatokeana Fresh tu,ila jamaa dizaini yuko Kenya..
Baada ya muda flani wa kuwasiliana wakakubaliana wawe wapenzi na kuahidiana kuonana soon...
Mwanaume akatimiza ahadi wiki chache zilizopita,akakwea pipa akaja Mwanza kumuona mchumba wa burebure aliyempata kupitia kwa hisani ya Mark Zuckerberg,owner wa mtandao huu wa Facebook..
Wamekula bata,imefika usiku wakakubaliana waende zao hotelini kula tunda bana...Kufika kule wameingia room...
UTAMU KOLEA
Walipochojoa mambo flani yanaitwa nguo yule msichana akagundua jamaa hayuko fresh kwenye sehemu za 'kinyume cha wazi',dizaini kama jamaa ameoza flani bwana...Demu akaona ah ah,hapa mechi haitachezeka bana...
Mshkaji akachomoa silaha na kutishia kumshoot kama ataondoka....Mungu jalia purukushani za hapa na pale yule msichana akafanikiwa kuchoropoka mikononi mwa mchizi...Akakimbia kwenda chuo..
Kufika chuo akawasimulia rafiki zake yaliyojiri huko hotelini.....
Ile kumaliza tu kuwasimulia...BALAA! Yule msichana hali yake ikabadilika akaanza kuoza bana,sehemu za 'kinyume cha wazi' kama jamaa...
Ikabidi wenzie wamkodishie Taxi kuwahi hospitali...ila sasa Cha ajabu...Kabla hawajafika mbali yule msichana akatoweka kwenye Mazingira ya kutatanisha...Yaani akayeyuka kabla hawajafika hospitali...
Mpaka habari hii inafika mikononi mwa ripota wa Blogu hii,huyo Msichana hajulikani alipo!
Inatisha...Dizaini jamaa ni mchawi au anatumia nguvu za kichawi na mwanafunzi ndio huyo amepotea na haijulikani nini kimetokea...
BE VERY CAREFUL....Haikatazwi kudate Facebook ila Just be Careful,you never know how dangerous the person you are messing with is....
Mi mwenyewe nimesisimka,ila imebidi nishee na wewe.....STAY SAFE!
Sehemu ya pili
Nimepata Fresh update mchana huu baada ya rafiki wa karibu wa Msichana huyu aliyepotea kunizamia hewani na kunipa mchapo mzima wa issue hii inayosisimua...
Stori ya jana iliishia kwa jamaa kumuita Msichana Hotelini ili waonane kwa mara ya kwanza na kucheza mechi matata....TUENDELEE
Alipo fika hotelini mshkaji alimuelekeza chumba alichopo akaenda akamkuta kalala, jamaa hakuamka kumkaribisha ,hamna cha waooooooo wala Hug... akasema njoo kitandani tu mimi nimechoka na uchovu wa safari
Basi Shosti akasema basi na mimi ngoja nioge ndo nije hapo kitandani si unajua kujiandaa na mechi tena
Akavua nguo akaingia bafuni kupiga ma-shower...
Wakati anatoka bafuni akamkuta jamaa kasimama,hayuko tena Kitandani...Halafu yuko uchi...Sehemu ya chini ya kitovu kuja kwenye eneo la tukio kuna kama Funza hivi wanatembea lakini hawaanguki chini...
Akataka kukimbia akamwambia ukikimbia tu unakufa, unataka kwenda wapi zile hela ulizokuwa unakula unadhani zilikuwa zinatoka wapi...Stori ni kwamba jamaa alikuwa anatuma mkwanja zaidi ya Laki3 kila mwezi kwa mtoto wa kike...Muda wa kuzilipia sasaaaa
Akamwambia haya panda kitandani unipe mambo mie...
Demu kusikia kufa akawa hana jinsi akapanda kitandani jamaa alivyosimika tu mzizi demu kama aka-pass out anakuja kushtuka kumekucha, haelewi nini kimetokea baada ya lile tendo...
Asubuhi ameamka anamuona jamaa kalala.....akikumbuka alicho kiona na wale funza na anavyo ona asubuhi hii ni tofauti... Mwanaume akawa wa kawaida kama anavyomuona Facebook,Handsome fresh tuu akaamka,akaoga freshi akamuaga mie naenda chuo basi ntakuja badae, akasepa
Basi kufika chuo hakutaka kuwaambia wenzie ukweli kwamba kapelekewa mjeledi na jamaa ameoza...Akauchuna akawaambia wenzie ameonana nae mshkaji...Ghafla akabanwa mkojo,kwenda chooni kukojoa anaona wale Funza kama jamaa kuleeeee....
Ikawa soo,ikabidi tu sasa aseme ukweli ili asaidiwe...Wenzie wakampeleka Dispensari ili asaidiwe...Kule akachomwa sindano lakini hali ikazidi kuwa mbaya ikabidi wale manesi wamshauri tu apelekwe Bugando Hospital wacheki zaidi tatizo.
Njiani kuelekea Bugando ndipo mazingaombwe yakatokea na demu akapotea ghafla...
Wale mashosti kwa kuwa walikuwa na namba za yule SHEMEJI JINI wakampigia simu ili kumuuliza kulikoni....Jamaa akasema WALA SIO YEYE NA HUYO ALIYEKUJA MWANZA HAMJUI....
No comments:
Post a Comment