Social Icons

Saturday 28 July 2012

Hoooot MWEZI MTUKUFU: Machangu wala Kichapo na Mboko za Nguvu huko Kinondoni ni Kutoka kwa kikundi cha Jumuia ya uamsho Tanzania Bara!!



WATUMIA BAJAJ
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.

BARABARA YA SHEKILANGO
Vijana hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya Sinza, Dar ambapo kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua mitaa ya Mwenge.

KINONDONI
Baada ya kufagiafagia Sinza kwa kuwaadabisha wanawake hao ndipo zoezi likahamia mitaa ya Kinondoni ambapo nao walipokea bakora za kutosha huku wengine wakitoka nduki.

KISA KUHARIBIWA SWAUMU 
Kwa mujibu wa vijana hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya muumini mmoja wa kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na kuvutwa kisha kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa swaumu yake.
Ilielezwa kuwa baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo kukatiza safari yake ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00 usiku.

Ilisemekana kuwa aliporudi nyumbani alitawadha na kufunga safari nyingine ya msikitini na alipofika kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo akawasimulia waumini wenzake ambao nao walikasirishwa na kitendo hicho hivyo wakapanga kuvamia maeneo yote ya biashara hiyo ili kuwashikisha adabu.
Waandishi wetu, wakiwa kwenye mishemishe zao za kutafuta habari mishale ya saa 5 usiku waliwashuhudia waumini hao wapatao saba wakishuka kwenye Bajaj nyeusi maeneo ya Sinza wakiwa na bakora mikononi kisha kuwavaa machangu hao na kuwatandika.
Wakati wakitekeleza zoezi hilo, jamaa hao walisikia wakiwaambia: “Sisi tupo kwenye swaumu nyiye mnatutega, ala!”

HAWAHESHIMU MWEZI MTUKUFU?
Waumini hao waliongeza kuwa makahaba hao wamekuwa hawaheshimu mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan ndiyo maana wanaendeleza biashara yao hiyo ya aibu.
www.globalpublishers.info

1 comment:

Anonymous said...

Huu ni unafiki mbona kabla ya mfungo hawa wadada hawachapwi bakora? si ndio hao hao wateja wao? kila mtu ashike dini yake