Social Icons

Friday, 20 July 2012

Kamera yangu ilimulika Miundombinu ya usafiri wa aina mbali mbali za Treni kwa wenzetu Nje.

TRENI LA KWANZA AMBALO LINAONGOZWA NA MITAMBO HAKUNA DEREVA NDANI
 Huu ni ubao maalumu unaoonesha safari mbalimbali, kwahiyo hauna haja ya kuuliza kila kitu kipo hapo
Hili ni eneo ambalo Treni hiyo ambayo inaongozwa na mitambo bila ya kuwa na dereva, inapita ni underground hapa, ambapo juu huko kuna majengo kibao, hapa milango imefungwa lakini Treni likiwasili tuu inafunguka
 Hapa Msimamizi wa Blog hii akiwa ametulia ndani ya Treni hiyo ambayo inatembea bila hata ya Dereva, kimsingi nikiwaga humu ndani nakuwaga na wasi wasi saana maana duuu balaa.

TRENI LA PILI: HILI NI TRENI AMBALO LINAFANYA SAFARI ZAKE TOKA MJINI MPAKA BUSHI
 Hapa msimamizi mkuu wa Libeneke hili nikiwa zangu ninapata ukodaki kabla ya kuingia katika Gogo ambalo ni zuri sana kwa ukweli
 Treni hili lina mabehewa kumi na sita, na huku yako matreni kama haya zaidi ya 30, ambayo yanafanya safari zake za kila siku, hili ni jipya kabisa. hili ni eneo la viti ambavyo ni kama makochi, full soft 
 Hapa nilipata nafasi ya kupata ukodak huku nikijaribu viti hivi vinavyo fanania, kiukweli ni vizuri sana 
 Hii ni aina nyengine ya viti hivyo ambavyo pia vina nafasi kubwa sana, abiria anaweza nyoosha miguu na kukaa bila ya kubanana
 Hizi ni alama ambazo zipo katika treni hili, sasa huku wadau ni vizuri kabla hauja kaa upitie pitie maana ukivunja sheria tuu unalo, kwa hiyo nyie wenye wapenzi mnaopenda mambo yetu yalee, tazameni sheria hapo
 Hivi ndivyo linavyo onekana kwa ndani ni full usafi hakuna mambo ya uchafu watu wanajiheshimu
Hii ni Tv ambayo inaonesha matangazo mafupi pia kuna, videofupi fupi ambazo zitakufanya usilale na zaidi, pembeni inakuonesha jinsi safari inavyo kwenda na kukuambia umefikia wapi. so hakuna konda wa kumuuliza tuko wapi, wala hakuna hajaya kuuliza kwa wadau kuwa umefika wapi.


 Hili Ndilo Treni lenyewe kwa nje sasa 
 Jii ni ramani inayo onesha sehemu zote unazo taka kwenda, hakuna haja ya kuuliza 

TRENI LA TATU: HILI NI TRENI AMBALO LINAKWENDA MWENDO KASI SANA KULIPO MAELEZO 
 Hapa ilikuwa muda mchache baada ya kuingia katika treni hii, nilikuwa nafanya kazi zangu za kublogisha kama kawaida bila hata ya ajiza, Hapa nilikuwa napost story flan ya jamaa.  kama unavyo ona pembeni kuna kajimeza ambao nimeweka simu yangu, pia nimeweka na notebook pamoja na bag ya kamera.
 Hivi ndivyo Gogo linavyo onekana kwa ndani
 Ndani ya Gogo hili la aina yake na lenye spidi ya ajabu sana, kuna mambo mengi sana ikiwa na kuwa na Free internet amabapo ni technolojia ya hali ya juu, wewe ukiingia tuu unaanza kutumia internet buree kabisa bila ya malipo yoyote yale. pia kuna TV ambazo zimesambaa treni zima 
 Hili ndilo Treni lenyewe hapa muda mchachache baada ya mimi kuwasili nako elekea, Kumbuka mimi ni mzurulaji sana ndio maana nawaletea vitu hadimu sana hapa kwa blog.

TRENI LILE LA PILI HAPO JUU: SASA HAPA NA MIMI NILISAFIRI KUELEKEA BUSHII HUKO HAPA NATOA DONDOO ZA USAFIRI NIKIFIKA PICHA ZITAFUATIA.
 Kwanza wakati safari yangu inaanza nilipanda hili treni jamani yani ni la zamaniiii kwa ukweli lakini sio kama ya Tanzania, hili la zamani kisasa, hapa ilikuwa tayari nimeshuka sasa naelekea huko porini. kwa ukweli hili Gogo Baya sana , tulikwama mara nne njiani, yani linazima zima, pia limejaa watu kibao sana, sasa AC ikikata ndipo kasheshe inaaanza na hakuna madirisha kufunguka. Sasa niambie hali inakuwaje hapo
 Kwa bahati  nzuri wakati nimemaliza Trip yagu huko country nilipata nafasi ya kupanda gogo Jipyaa.. yaani ndani ya treni hili full burudanii kwa kweli, Lakini lazima uwe unajua kusoma maana usije chekwa soma hapo wameandikaje? kisha utafuata 
 Huu ndio muonekano wa treni hilo
 Sasa hapa Treni hilo lilikuwa linawasili  kuchukua abiria wengine
 Hapa  nilikuwa nangoja Treni kuelekea Huko Selembani ambapo picha zinakuja, nikitokea Legenda ambapo pia picha zinakuja baadae.
Nilipata ukodaki nikiwa steshen za Legenda 
Hapa Bado nangoja Treni lije nipate endelea na mizunguko yangu, sisi wazururaji hatutumii private, tunatumia public transport kujua muji vema

 Hapa Treni letu limewasili na Mwendo mdundo 
 Wakati huo kuna Gogo linatoka Ipoh kuelekea town


 Kibao cha steshen
Kasheshe lilianzia hapa sasa ambapo Treni langu la kutoka Selemban kuelekea town lilichelewa sana, sasa hapa mimi ja mshikaji pembeni tulikuwa tumechoka balaa.
Hii ilikuwa ni picha ya mwisho ambapo kamera mani alinikamua nikiwa nimelala Choka mbaya sana, na baada ya hapo kamera iliishiwa na Betrii, hivyo kukawa hakuna tena kukamua picha.

Hope wadau mtakuwa mmeenjoy sana kuona jinsi gani wenzetu wameendelea katika secta nzima ya miundo mbinu hasa katika hili la Treni, Picha zote nimepiga mimi kasoro hiyo ya mwisho tuu. Huwa nina Timing zangu ndio maana.

Endelea kufuatilia maana bado kuna maeneo mbali mbali yanakuja kadili siku zinavyo enda.. 

No comments: