Social Icons

Saturday, 14 July 2012

Trip yangu ya Indian Temple Batu Caves Gombak

Kwanza Kabisa unapo ingia hapa unakaribishwa na Mungu wao wa Kihindi ambae wametengeneza Bonge la Sanamu la Gold Polished.
 Hapa ndio mwonekano wakati wa kujiandaa kuingia katika Caves, Ngazi hizo hapo juu zipo zaidi ya 270 ambapo unatakiwa kuzimaliza ndio ufike Pangoni
 Muda Mchache baada ya mimi kuwasili katika eneo hilo 
 Hizi Ni baadhi ya Tempo ndogo za wahindi katika eneo hilo 
 Baadhi ya maeneo ya kuvutia sana katika eneo hilo 
 Kwa mbali sana ni muonekano wa pango hilo 
 Hapa sasa ni ndani ya pango hilo kubwa ambalo limesheena mambo kibao ya utamaduni wa kihindi 
 Baadhi ya Miungu ya wahindi 
 Nilipata kupiga picha katika moja ya miungu wakubwa wa Kihindi, katika tempo hiyo iliyopo Gombak 
 Nilipo kuwa huko naendelea na trip yangu nilikutana na Rafiki yangu anaitwa Bella nae alikuja katika mishe zake za kutazama tempo
 Hapa pia kwa Wahindi wanajua ni baadhi ya Miungu yao wanayo iabudu 
 Watu kibao eneo hili hapa ambapo wamekuja kutembelea na kuona nini kinaendelea, hapa choka mbaya maana nawaza kushuka ngazi.
 Huku ni Juu kabisa Pangoni ambapo kuna mambo kibao ambayo kwa kweli yanavutia sana.
 Nyani pia wapo sana tuu lakini ni mabeste hawana shida na mtu 
 Hapa nilikuwa nje ya Bwawa ambapo kuna mambo kibao ndani wakiwemo samaki wa kila aina 
 Nikiwa kwa Tempo 
 Baada ya kuzunguka nilikutana na hii hapa sijui ina maanisha nini 
 Hii ni Moja ya sehemu ambayo wahindi hufika hapa na kuanza kuabudu 
 Kuna kitu kimoja kinafurahisaha sana hapa, hawa njiwa wapo wengi sana na hawaogopi watu kimeonekeana ni moja ya vivutio sana katika eneo hili nikaona vema nipate ukodak 

 Hapa Nilipata muda wa kufanya zoezi la kuabudu ingawa ilikuwa ngumu sana
Baada ya hapo nilimalizia Tripyangu hapa 

****

No comments: